Naibu mkuu
wa Takukuru Mkoa wa Pwani Sadiki
Nombo akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake akitoa taariga kuhusiana na utekelezaji wa kazi amabzo
wamezifanya katika kipindi cha kuanzia mwezi Octoba hadi disemba mwaka
huu. (Picha na Victor Masangu).
VICTOR MASANGU, PWANI
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU ) Mkoa wa Pwani imefanikiwa kuokoa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 58 ambazo zimetokana na malalamiko yaliyowasilishwa yakiwemo ya wimbi la ubadhilifu wa fedha ambazo wamedhulumiwa wakulima wa zao la korosho ikiwemo na vikundi vya vijana wanawake na walemavu.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Naibu mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Sadiki Nombo kwa ajili ya kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ambayo yameyafanya kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita kuanzia mwezi Octoba hadi kufikia Disemba mwaka 2020 pamoja na mikakati waliyojiweke katika kukabliana na wimbi la rushwa.
Aidha alifafanua kuwa katika robo ya kuanzia mwezi octoba hadi disemba mwaka 2020 Ofisi ya Takukuru iliweza kupokea mamalamiko yapatayo 196 ambapo kati ya hayo malalamiko 113 uchunguzi wake bado endelea kufanyika ili kuweza kuwabaini wale wote waliohusika na sheria iweze kufuata mkondo wake.
Pia aliingeza kuwa katika utekelezaji huo Takukuru Wilaya ya Mkuranga waliweza kukoka kiasi cha shilingi milioni 18 ambazo zilizotoka na baadhi ya wakulima kudhulumiwa na viongozi wa bodi ya Amcos ya kimanzichana kusini.
Kadhalika katika Wilaya ya Kibiti Takukuru iliweza kuokoa kiasi cha shilingi zaidi ya shilingi milioni 18 ambazo ziliweza kuokolewa kutoka katika vikundi mbali mbali ikiwemo kwa vijana, wanawake pamoja na walemavu ambavyo vilikopeshwa na halmashauri hiyo kushindwa kurejesha mikopo hiyo.
Aidha alifafanua kuwa kupitia katika Ofisi ya Wilaya ya Kisarawe waliweza kufanya uchunguzi wa kina na kuweza kuokoa jumla ya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni nne amabzo ziliweza kuchangwa na wananchi wa kijiji cha Marui Ngwata kwa ajili ya kufanya ujenzi wa mradi wa zahanati ya kijiji hicho.
Kwa upande wa Ofisi ya Chalinze katika kipindi cha mwezi octoba hadi disemba mwaka 2020 iliweza kufanikia kurejesha kiasi cha shilingi milioni moja zikiwa ni sehemu ya shilingi milioni tano amabzo zimetokana na mikopo amabyo ilitolea kwa vikundi vya wanawake vijana pamoja na watu wenye ulemavu.
Ofisi ya Takukuru Wilaya ya Kibaha waliweza kufanya uchunguzi na kuweza kuokoa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni tisa kutoka kwa wanunuzi wa dawa za kituo cha afya cha mlandizi ambapo manunuzi hayo yalikiukwa na utaratibu haukuzingatiwa ipaswavyo kwani dawa ziliozagizwa kutoka kampuni binafsi ya Astra Pharma Limited.
Katika hatua nyingine Naibu huyo alibainisha kwamba Takukuru katika kupambana vilivyo na wimbi la rushwa ya ngono ambayo imeonekana kuwa ni chngamoto kubwa katika baadhi ya maeneo hususan kwa wanafunzi wameanzisha kampeni maalumu ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kupunguza hali hiyo.
Takukuru Mkoa wa Pwani katika robo ya tatu kuanzia mwezi octoba hadi disemba mwaka 2020 imeweza kupokea kesi zipatazo 27 ambazo zinaendelea kusikilizwa katika mahakama mbali mbali pamoja na kupokea malalamiko yapatayo 196 ambapo kati ya hayo malalamiko 113 yapo katika hatua ya uchunguzi.
No comments:
Post a Comment