Na Zuena Msuya, Pwani
Watumishi wa Wizara ya Nishati, wamesema kuwa wamefurahia sana ziara ya kutembelea Mradi wa kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere(JNHPP) Mkoani Pwani.
Ziara hiyo ya Siku tatu imeratibiwa na Uongozi wa Wizara ikisimamiwa na msimamizi wa Mradi huo kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Christopher Bitesigirwe kwa kushirikisha watumishi kutoka Idara na vitengo mbalimbali vya wizara hiyo.
Wamesema kuwa ziara hiyo imekuja wakati muafaka na imekuwa na ufanisi mkubwa kwa kuwa wamejifunza na kujionea hali halisi ya kinachoendelea katika mradi huo.
Watumishi hao wamesema kuwa wanaushukuru sana Uongozi mzima wa Wizara kwa kuridhia na kuwawezesha watumishi wake kutembelea mradi huo pamoja na yule aliyetoa wazo la watumishi kutembelea mradi huo na waliounga mkono.
" Sisi watumishi tunajisikia fahari na kujivunia sana kwa kuwa sehemu ya mradi huu kwa kuuona kwa macho yetu na vitendo, utekelezaji wake tangu hatua za awali na si kwa maandishi wala kusimuliwa,
Hakika tutapata cha kueleza vizazi vyetu hapo baadaye ", Walisema Watumishi hao.
Watumishi hao walienda mbali zaidi kwa kusema kuwa, huo ni mwanzo mzuri kwa Wizara yao, na wanaimani itaendelea kuwashirikisha kwa kuwapa ridhaa ya kutembelea katika miradi mingine inayoendelea kutekelezwa.
Hata hivyo walieleza kuwa utaratibu huo umeongeza chachu ya kuitendaji kwa watumishi hao kufanya kazi kwa kasi kubwa, Ubunifu, Umakini zaidi na kwa usahihi na kujiona ni sehemu ya Mradi huo.
Ziara hiyo ya Siku tatu inahusisha Watumishi wote wa Wizara ya Nishati kutoka Idara na Vitengo mbalimbali ambao hutembelea mradi huo kwa awamu tofauti na katika Makundi.
January 31, 2021
Home
Unlabelled
Watumishi wa Nishati wafurahia kutembelea mradi wa JNHPP
Watumishi wa Nishati wafurahia kutembelea mradi wa JNHPP
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment