Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda akizungumza na madiwani na wabunge wa CCM mkoa wa Iringa wakati wa semina elekezi.
NA DENIS MLOWE, IRINGA
WAZIRI
MKUU Mstaafu na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa
Mizengo Pinda amewaagiza viongozi katika ngazi mbalimbali mkoani Iringa
ambao walichaguliwa kwa tiketi ya chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu
uliopita kwenda kuisimamia Ilani kwa kushughulikia changamoto za
wananchi waliowachagua.
Akizungumza
katika Semina Elekezi iliyohusisha wabunge wote na madiwani wote wa CCM
Mkoa wa Iringa na kufanyika katika ukumbi wa CCM mkoa wa Iringa,
Mizengo Pinda alisema imani ambayo wananchi wamekionyesha chama hicho
kwenye Uchaguzi Mkuu na kuwapa ushindi mkubwa ni kubwa na ina stahili
kulipwa kwa kuwatumikia wananchi kama ambavyo imeainishwa kwenye Ilani
ya chama.
Alisema kuwa wananchi
wamekipa imani chama cha Mapinduzi na sasa ni zamu ya waliochaguliwa
kuwaletea maendeleo ambayo wananchi wanayasubiri kwa hamu kubwa na
ikumbukwe kwamba mbunge au diwani ambaye hatafanya kazi kwa misingi
ilani ya chama katika kuwaletea maendeleo wananchi anawapa kazi kubwa
chama kuweza kushinda katika chaguzi zake.
Aidha
Pinda alisema kuwa chama kinatakiwa kutembelea miradi yote ambayo
serikali inatekeleza kwenye maeneo ya wananchi kwani usipofanya hivyo
huko kwenye kata wananchi kuna malalamiko mengi na unakuta diwani hata
kwenye mradi mmoja hajafika hapo utakuwa diwani wa ajabu sana.
"Lazima
twende kutembelea miradi kuona ile ilani ambayo wananchi walielezwa
kwenye kampeni inakwenda inavyotakiwa? tukifanya hayo ndugu zangu
tutaona sehemu kubwa kabisa tutafanya kazi ya chama kuwa nyepesi na
kurahisha shughuli katika chaguzi zinazofata" alisema
Aliongeza
kuwa wabunge au madiwani kufanya ziara kwenye maeneo yao ni lazima
isitokee kiongozi anasema kuwa asipangiwe shughuli za kufanya kumbuka
chama kina taratibu zake na chama kikiona hufanyi kazi vizuri hakiwezi
kukuacha hivi hivi kwani lazima chama kimbane mbunge kuhakikisha
anafanya ziara kwenda kusikiliza changamoto za watu ,kuyapatia ufumbuzi
na aweke utaratibu wa kusikiliza kero za watu kila wiki au kila
anapopata muda.
Alisema kuwa
kama mbunge au diwani hafanyi kazi yake ipasavyo ndio chanzo cha rais
Magufuli kufikishiwa barua nyingi ambazo hazina sababu kwa sababu wa
chini yake hawafanyi kazi ipasavyo hivyo ni wajibu wa kila mbunge na
diwani kufanya hivyo kusikiliza kero za wananchi.
Alisema
kuwa ukifanya wajibu wako wa kukutana na makundi ambayo yamesaidia kwa
kiasi kikubwa kufanikisha ushindi na kusikiliza kero zao na sio kama
ilivyo kuwatafuta kipindi cha uchaguzi kisha wakati huku mwanzo ulikaa
kimya hiyo safari hii kama chama hakiwezi kuvumilia.
Pinda
alitoa wito kwa viongozi kuhakikisha sekta binafsi kutoiweka pembeni
katika maendeleo ya nchi hivyo ndani ya chama tawala tuone namna gani
sekta binafsi inapata nafasi ya kusikilizwa kila mara kwa lengo la kuona
changamoto wanazokabiliana nazo ili kuziondoa.
Aidha
alitoa wito kwa viongozi kuhakikisha wanasoma ilani kwa umakini ili
kuweza kubaini ahadi za wananchi katika kuwaletea maendeleo hivyo
wananchi wanategemea mengi kutoka ndani ya chama cha Mapinduzi
walichokipa madaraka ya kuongoza dora.
akizungumzia
kuhusu mapato ya chama Pinda alisema kuwa bado inahitajika nguvu kubwa
katika kukiletea mapato chama kwani inahitajika kazi kubwa na kuwataka
makatibu kusimamia makusanyo ya mapato kila mkoa ili kukifanya chama
kiweze kujitegemea iwe ajenda ya watu wote wakiwemo wabunge na madiwani
kiwe kinajitegemea.
Aliwataka
kuhakikisha miradi iliyopo inasimamiwa vizuri kila kinachopatikana
kiende kikafanye kazi ya kujenga chama hivyo wale wenye tabia ya
kukusanya fedha na kuingia mfukoni waache mara moja kwani hadi majuzi
hapa kuna taarifa kuna baadhi wanakula fedha za chama hivyo lazima kuwe
na miradi katika ngazi ya kata,ngazi ya tawi lazima hata kama midogo
itasaidia.
Aidha alisema kuwa
mafunzo kwa viongozi na makada ni muhimu sana yanasaidia kukumbushana
mambo mbalimbali ya uongozi kuliko kukaa bila mafunzo na kuwaacha
viongozi kutoelewa suala zima la kuongoza.
Kwa
upande wake Mwenyekit wa CCM Mkoa wa Iringa Dk Abel Nyamahanga alisema
wao kama chama watapita katika maeneo mbalimbali kuangalia utekelezaji
wa ilani na kamwe hawatakuwa na simile na kiongozi atakayeshindwa
kutekeleza kwa vitendo ahadi alizozitoa kwa wananchi kipindi cha
uchaguzi.
Kwa upande wao baadhi
ya wabunge akiwemo Justin Nyamoga Mbunge wa jimbo la Kilolo alisema kuwa
maagizo waliyopewa na watayafanyia kazi kwa lengo la kuwaletea
maendeleo wananchi na kuhakikisha ahadi zote zinafanyiwa kazi.
Nyamoga
alisema kuwa semina hiyo imewejenga kwa kiasi kikubwa kwani
inawakumbusha kwamba wale wote waliochaguliwa wana deni kubwa kwa
wananchi na endapo wakizembea katika kuwatumikia wananchi kutakuwa na
kazi kubwa sana katika chaguzi zijazo,
"wananchi
wametupa imani kubwa sana na ndio maana tukaibuka na ushindi wa
kishindo katika chaguzi iliyopita hivyo deni hili linalipwa kwa
kuwaletea maendeleo wananchi waliotuchagua na kumpa kura za kishindo
rais Magufuli" alisema.
No comments:
Post a Comment