HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 25, 2021

Waziri wa Kilimo abaini ushindani hafifu zao la Tumbaku

 HAMIDA RAMADHANI, DODOMA


WAZIRI wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa bado kuna changamoto katika zao la Tumbaku hasa kwenye suala zima la ushindani wa ununuzi wa zao hilo.

Waziri Mkenda ameyasema hayo leo jijini hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha ndani na Bodi ya Tumbaku.

Amesema licha ya Bodi ya Tumbaku kufanya vizuri katika suala zima la ushindani wa ununuzi wa zao hilo kwani liko chini ,hivyo hawana budi kuongeza  juhudi  za  Mazingira ya ushindani katika soko.

Amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 zinazolima na kuzalisha zao la Tumbaku huku changamoto kubwa ikiwa ni kiwango kidogo cha ushindani.

 "Tumbaku ni  zao linaloliingizia Taifa  fedha nyingi za kigeni kwa mwaka USD Milioni 285 tofauti na mazao mengine  yanayolimwa hapa Nchi  ambavyo nayo ni  mazao ya kimkakati," amesema Mkenda.

" Haiwezekani Tumbaku ilimwe Tanzania ipelekwe Nchini Zambia kule kwani Zambia inapata bei nzuri halafu wanairudisha tena Tanzania nasisi ndio tuuze nchi za nje hapana tumechoka Tanzania kuonekana ni shamba la bibi," amesema.

" Zao la Tumbaku litaendelea kuwa zao namba moja la uchumi hapa Nchini Tanzanian amesema Waziri Wa Kilimo Mkenda. 

Na kuongeza kusema " Kunatabia ya Baadhi ya wanunuzi kudai kuwa hawanunui tumbaku yote inayozalishwa nchini na mikataba ya ununuzi  ni michache kuliko tumbaku inayozalishwa 

Amesema Tumbaku nyingi ya Tanzania inayobaki inauzwa kwa makinikia (ulanguzi) na soko limehamia zambia kwa  kupeleka tumbaku ya Tanzania kwenye soko la zambia kwa magendo na kisha inarudi tena kusafirisha kupitia bandari ya Tanzania 

Pia ameitaka Bodi itoe majibu ya kitaalamu kwa nini Hali hiyo inajitokeza na itoe sababu za Kufungwa kwa kiwanda cha kusindika tumbaku kilichopo Morogoro

Pia amesema katika  kulinusuru soko la bidhaa hiyo Tanzania inafanya mazungumzo na mataifa ya misri na China na indonesia Ili kununua tumbaku inayozalishwa nchini badala ya kutegemea makampuni yanayohodhi soko la tumbaku duniani ambayo ni manne tu.

No comments:

Post a Comment

Pages