HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 23, 2021

KAGERA YAWEKA REKODI YA UZALISHAJI KAHAWA GHAFI

 

 

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

 

 Na Lydia Lugakila, Bukoba

Mkoa wa Kagera umekusudia kufikia wastani wa kilo milioni 100 katika uvunaji kahawa, huku msimu huu wa mwaka  2020-2021 mkoa huo umefanikiwa  kuweka rekodi ya uzalishaji wa kahawa ghafi ya kilo milioni 78.3.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti wakati akiongea na waandishi wa Habari ofisini kwake.

Marco Gaguti amesema mkoa huo umeweka rekodi ya uzalishaji wa kahawa ghafi ya kilo milioni 78.3 Jambo ambalo limeuweka Mkoa huo katika historia ya zaidi ya miaka 10 kwani hakuna ambapo mkoa huo ulifanikisha wakulima kuvuna kahawa nyingi kiasi hicho, kwani msimu uliopita walifanikiwa kupata kilo milioni 52 huku msimu uliotanguliwa  2018- 2019 ilikuwa milioni 58.

Akijata mafanikio yaliyopatikana katika ukusanyaji na uuzaji wa kahawa kwa msimu ambao umeisha Brigedia Gaguti amesema yametokana na jitihada za wakulima wenyewe kuendelea kuboresha mashamba yao, kampeini mbali mbali ambazo zimekuwa zikifanyika katika ngazi ya mkoa ambapo wakulima wameitikia wito na kianza kupanda mbegu zenye tija zaidi.

Amesema historia hii ya mafanikio imekuja kufuatia kuzuia wimbi kubwa la magendo kwani miaka ya nyuma kahawa hiyo ilikuwa inavushwa kwenda nchi jirani ambapo kazi kubwa iliyofanyika ilikuwa ni kuanza kuimalisha doria ili kuhakikisha kahawa na Mali nyingine hazivuki mipaka, kubwa zaidi ikiwa ni upatikanaji wa fedha  ambao umesaidia kuhakikisha wananchi hawavutiwi na kuiuza kahawa katika maeneo mengine ya nchi, pamoja na fedha za wakulima kupatikana kwa wakati.

"Hii  ni rekodi kubwa nitumie fulsa hii kuwapongeza wakulima wa mkoa wa Kagera lakini pia niwaombe wadau wote  wa kahawa wakati msimu mpya unakaribia kuanza lindeni mafanikio ambayo yamepatikana kwa kuhakikisha mnaendelea kutumia mbinu na njia bora zaidi za kilimo na kuboresha mashamba, kutunza kahawa kuanzia shambani mpaka sokoni ili kahawa iendelee kuwa na ubora ambao ni wa viwango vya kimataifa" alisema Brigedia Gaguti.

Aidha amesema kwa msimu wa 2021- 2022 unaotarajia kuanza mwaka huu mwezi wa 5 au 6 Mkoa huo utadumisha mafanikio hayo na kupiga hatua zaidi huku akiwaomba wote wanaohusika na cheni ya mnyororo wa thamani wa kahawa wanashirikiana ili mtu wa kwanza kulindwa awe ni mkulima.

Ameipongeza Benki ya TADB na wadau wengineo kwa kufanikisha agenda hiyo na kuwataka wadau hao kujipanga mapema ili maandalizi yaanze na kuruhusu wakulima ili wanufaike na jasho lao.

Mkuu huyo wa mkoa ameongeza kuwa atapenda kuona msimu utakaoanza wakulima wanapata fedha zao kwa muda mfupi zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka 2020 ambapo tayari alishakaa kikao cha wadau ili kuweka maadhimio maalum ya kuhakikisha mkulima anaweza kulindwa na kuwataka wakulima hao kutumia kipindi cha mvua kuhakikisha mbegu hizo zinatunzwa ambapo lengo la Mkoa katika mpango wa  muda mrefu  ni kufikia angalau kilo milioni 2 au tani laki 2 kwa mwaka.

Hata hivyo amewataka watanzania kuendelea kufikilia kuwekeza katika kuongeza thamani ya mazao hasa zao la kahawa ambapo kwa Sasa bado kawaha inauzwa nje ki ughafi chini ya asilimia 10.

No comments:

Post a Comment

Pages