Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine
Ndugulile (wa pili kushoto), akionyesha SimBanking mpya inavyoonekana baada ya
kujiunga wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, uliofanyika jijini Dar es Salaam
jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela na wa
pili kulia ni Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Prof. Neema Mori na kulia
ni Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA), Khadija Said. (Na
Mpiga Picha Wetu).
Waziri wa
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile (wa pili kushoto),
akizindua huduma mpya ya SimBanking inayowawezesha watanzania kufungua akaunti
popote walipo kupitia simu ya mkononi, uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es
Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid
Nsekela na kulia ni Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Prof. Neema
Mori. (Na Mpiga Picha Wetu).
NA IRENE MARK
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile amezitaka benki nyingine hapa nchini kuiga mfano wa huduma bora za kiteknolojia zinazotolewa na Benki ya CRDB wakati huu wa kuelekea kwenye Tanzania ya TEHAMA.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa huduma wa SimBanking iliyoboreshwa, aliupongeza uongozi wa Benki ya CRDB kwa kuboresha huduma zake kwenye TEHAMA na kuwafikia wateja wake popote kwa wakati wote.
Dk. Ndugulile alisema lengo la Rais John Magufuli kuunda wizara maalum ya TEHAMA ni kuigikisha Tanzania kwenye ulimwengu wa teknolojia hivyo ipo kazi kubwa ya taasisi kuondokana na mazoea ya utoaji huduma kwa wananchi.
“Mheshimiwa Rais ametupa kazi kubwa ya kufanya kwenye wizara yetu maana tunatakiwa kuipeleka Tanzania kwenye ulimwengu wa TEHAMA.
“Nitoe rai kwa benki nyingine, kuiga sio dhambi... nao waige kwa Benki ya CRDB yaani mteja anauwezo wa kufanya kila kitu kinachohusu akaunti yake na zaidi akiwa na simu yake ya mkononi.
“Benki ya CRDB wamenifariji zaidi baada ya kujua kwamba waliounganisha huduma za kibenki na simu za mkononi ni vijana wa kitanzania yaani ‘local services’ hili nalo ni jambo la kupongeza sana.
“...Hata serikali hivi sasa inawafuata wananchi kwa kuhakikisha masuala yote ya malipo ya serikali yanafanyika kwa simu za mkononi,” alisema Dk. Ndugulile ambaye pia ni Mbunge wa Kigamboni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema lengo la taasisi hiyo kubwa ya fedha hapa Tanzania ni kumfikia mwananchi popote alipo kwa kutumia wataalam wazalendo.
“Tumejipanga vizuri kupitia kitengo chetu cha teknolojia kinachoongozwa na vijana wazalendo kuhakikisha Benki ya CRDB inakuwa kinara wa teknolojia katika utoaji wa huduma zetu,” alisema Nsekela.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Khadija Said aliipongeza Benki ya CRDB kwa ubunifu bora wa huduma za kiteknolojia na kuwawezesha wateja wa benki hiyo kukata bima mbalimbali kwa kutumia simu ya mkononi.

No comments:
Post a Comment