HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 11, 2021

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUNGUA SOKO KUU LA MKOA WA MOROGORO (MOROGORO CENTRAL MARKET)

Soko Kuu la mkoa wa Morogoro kama linavyoonekana mara baada ya kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 11 Februari 2021. PICHA NA IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo kuhusu changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo wafanyabiashara hao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyabiashara mbalimbali wa Soko Kuu la mkoa wa Morogoro ili kujua changamoto zao mara baada ya kulifungua Soko hilo katika Manispaa ya Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyabiashara mbalimbali wa Soko Kuu la mkoa wa Morogoro ili kujua changamoto zao mara baada ya kulifungua Soko hilo katika Manispaa ya Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kufungua Soko Kuu la Morogoro pamoja na Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare, Mbunge wa Morogoro mjini Aziz Abood pamoja na viongozi wengine wa mkoa wa Morogoro.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli  akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Morogoro mara baada ya kuzindua Soko Kuu la mkoa huo leo tarehe 11 Februari 2021.

No comments:

Post a Comment

Pages