Mkuu wa Takukuru Dodoma Sosthenes Kibwengo.
Fedha zilizorejeshwa.
NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA
TAASISI
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma imefanikiwa
kurejesha Jumla ya Shilingi Milioni 176,565,000 pamoja na nyumba moja
kwa walimu wastaafu ambao walilipishwa fedha hizo na kunyang'anywa na
bwana mapesa kinyume na utaratibu.
Kutokana
na hayo wito umetolewa kwa wakopeshaji wa fedha mkoani hapa kuzingatia kanuni na taratibu za nchi na kuacha tabia ya kuwatoza wananchi riba
umiza.
Walimu hao
wastaafu waliochukuliwa mali na fedha zao na kampuni ya GENEVA CREDIT
SHOP inayomilikiwa na Abubakari Kinyuma maarufu kama Abubakari
Mapesa iliyopo mjini Kondoa mkoani hapa.
Akizungumza
na waandishi wa Habari leo Mkuu wa Taasisi hiyo mkoani hapa, Sosthenes Kibwengo, amesema baada ya kufanyia uchunguzi kampuni hiyo
mwezi Januari 2021walibaini kuwa mmiliki wa kampuni hiyo hukopesha fedha
kwa riba kubwa ambapo imepelekea wananchi kumlalamikia kutoka na mikopo
umiza anayoitoa.
"Kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wataendelea kukokota
kiasi cha kodi ambacho kampuni hiyo inadaiwa huku ikiendelea kufuatilia
shilingi milioni 184,586,000 za wakopeshaji 22 ambazo zinapaswa
kurejeshwa na Bwana mapesa," Amesema Mkuu huyo Kibwengo.
Wakizungumza
Mara baada ya kurejeshwa fedha zao wananchi hao wameishukuru taasisi
hiyo kwa kuwasaidia kupata fedha zao ambazo zilichukuliwa na Bwana
Mapesa kwa kuongezeka riba kubwa .
Hata hivyo
wananchi wameombwa kujihadhari na mikopo umiza na kamwa wasikubali
kumkabidhi kadi zao za benki au hatua za nyumba kwa mtu yeyote .
No comments:
Post a Comment