HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 14, 2021

WANAFUNZI ELIMU YA JUU WAPATA MAFUNZO YA UFUGAJI JONGOO WA PWANI ZANZIBAR

 

 

Ni masomo kwa vitendo, wanafunzi wa vyuo vikuu Zanzibar wakiwemo wa SUZA na wengine wamejikubalisha kuja katika shamba hili kujionea uhalisia kama inavyoonekana maafisa wa Wakulima hai Cooperative Society wakiendelea na masomo ya namna unavyoweza kumfuga jongoo wa pwani.

Mwenyekiti wa Wakulima hai, Ndg Daud Mohamedi akiwafundisha wanafunzi kiwango cha chumvi maalum kinachotakiwa ili jongoo aweze kuishi na kukua vizuri, mkononi amekamata kifaa maalum cha kupimia chumvi ya baharini.
Katibu wa Ushirika wa Wakulima hai Bi Semeni Mohamedi akimuonesha mwandishi wa habari aina moja ya Jongoo la Pwani ikiwa ni sehemu ya mafunzo wanayopatiwa wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini juu ya ufugaji wa majongoo ya pwani na kujikuza kiuchumi.
 

No comments:

Post a Comment

Pages