Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy
Gwajima (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu matukio ya ukatili nchini. (Picha na Hamida Ramadhani).
NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA
WAZIRI
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy
Gwajima amewataka wanaume kutoa taarifa kwenye mamlaka husika kuhusu
ukatili wanaofanyiwa ili kutokomeza matukio ya ukatili nchini.
Dkt.
Gwajima ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma alipotoa tamko kuhusu
Vitendo vya Ukatili katika jamii mbele ya waandishi wa habari.
Gwajima
amesema vitendo vya ukatili vimezidi kuongezeka hapa nchini akitolea
mifano mbalimbali iliyotokea hivi karibuni ya waanfamilia kufanyiana
vitendo vya kikatili.
Amesema
ukatili haufanywi kwa wanawake na watoto tu lakini hata kwa makundi
mengine ikiwemo wanaume lakini wengi wao wamekuwa wakinakaa kimya.
"Wanaume
msione aibu, muache kukaa kimya dhidi ya vitendo vya ukatili
mnavyofanyiwa. Toeni taarifa mapema kwa mamlaka husika muweze kupata
msaada ili kuzuia madhara zaidi kutokea" amesema Gwajima.
Amezitaja
sababu za ukatili huu ni pamoja na migogoro ya kifamilia ikiwemo
kugombea mali, matatizo ya kisaikolojia na jamii kutotekeleza wajibu
wake wa kutunza na kuimarisha ulinzi kuanzia ngazi ya familia.
Dkt
Gwajima amesema Wizara itaendelea kuchukua jitihada zote kuhakikisha
ukatili unatokomezwa kwa makundi yote, lakini jamii pia ina jukumu la
kuwalinda makundi yote.
Aidha,
amesema Wizara itaendelea kushughulikia mauaji ya wazee na kuwa
haitorudi nyuma kupambana na ukatili wa aina yoyote ili nchi na mipaka
yake ibaki salama kwa amani, upendo na kujiletea maendeleo.
Naye
Afisa Ustawi Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Amina Mafita amesema
Wizara imejikita zaidi katika kuelimisha jamii kwa kuunda mabaraza
kuanzia ngazi za vijiji na mitaa kwa lengo la kulinda makundi yote.
No comments:
Post a Comment