HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 13, 2021

WAUZAJI SENENE WATAKIWA KUJISAJILI TBS



Na Lydia Lugakila, Bukoba

 
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Ziwa mkoani Kagera imewataka wajasiriamali mbalimbali wakiwemo wauzaji wa senene kujisajili ili kuwezesha biashara yao kuwa na alama ya ubora ili kuwapa uhakika wanunuaji toka ndani na nje ya mkoa huo kununua biashara yao  bila kutilia mashaka.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Uthibiti Ubora Kanda ya Ziwa, Vicent Mabula, wakati akizungumza na wajasiriamali mbalimbali wakiwemo wa mboga mboga, wauzaji wa senene, wakulima katika tamasha la SENENE FESTIVAL 2021 yenye lengo la kuongeza thamani ya kupanua masoko lililofanyika katika ukumbi wa ELCT Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Vicent amesema kuwa biashara yenye alama au nembo ya TBS huaminika  na kwenda hadi nje ya nchi kutokana na kuwa  na ubora wenye viwango.

Aidha ameongeza kuwa kutokana na biashara ya senene kuonekana kupendwa na watumiaji, jambo linaloweza kuleta wasiwasi kwa watumiaji toka ndani na hata nje ya mkoa baada ya kutaka kununua bidhaa hiyo na kukuta aina viwango toka TBS na kufanya biashara hiyo kushuka thamani.

Akitaja faida za viwango mwakilishi TBS amesema kuwa huweka usawa katika uwanja wa biashara, uondoa mkanganyiko kuhusiana na bidhaa, husaidia kufungua masoko zaidi, huraisisha biashara baina ya nchi na nchi ikiwemo kutoa uhakikisho wa ubora, usalama, kuaminika na ufanisi pamoja na kulinda afya na usalama wa walaji au watumiaji wa bidhaa mbalimbali.

Amewataka wajasiriamali hao kufanya utaratibu wa kusajili bidhaa zao ili kuwa katika viwango vya kitaifa na kimataifa.

Hata hivyo kwa upande wake Josephina Ansibert mfanyabiashara wa Senene ameishukuru TBS kwa kutoa mafunzo hayo kwa wajasiriamali hao huku akikiri kuwa kwake ilikuwa mara ya kwanza kusikia TBS na kueleza kuwa kwa sasa anaweza kuboresha Senene wake katika kiwango ili kuuzwa  kitaifa na kimataifa .

No comments:

Post a Comment

Pages