Na Catherine Sungura, WAMJW-Dodoma
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea
kuratibu uanzishwaji wa madawati ya Ulinzi wa Watoto katika shule za
msingi na sekondari nchini.
Hayo
yamesemwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji
wa majukumu ya Wizara (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kwa kipindi
Cha Julai,2020 hadi Februari, 2021.
Dkt.
Gwajima amesema hadi kufikia Februari,2021 jumla ya madawati 182
yameanzishwa na jumla ya wasimamizi wa madawati shuleni wapatao 360
walipatiwa mafunzo ya namna ya kusimamia madawati hayo ili kupunguza
ukatili wa Watoto shuleni.
"Katika
kutokomeza mila na desturi zenye madhara zinazosababisha kuongezeka kwa
vitendo vya ukatili dhidi ya Watoto nchini, Wizara tumetoa elimu kuhusu
athari za Mila hizo kwa Watoto, wananchi, walimu pamoja na viongozi wa
kisiasa, dini na wale wa kimila katika Mikoa ya
Mara,Geita,Tanga,Rukwa,Mbeya na Kigoma". alisema Dkt. Gwajima
Kwa
upande wa kutokomeza mimba za utotoni Dkt. Gwajima alisema wameweza
kuwafikia wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa kuwapatia uelewa
kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni kiafya, kielimu na kiuchumi
pamoja na kuzuia ukatili mtandaoni.
Katika
hatua nyingine ya taarifa ya utekelezaji ya Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii hususan katika kuwawezesha Wanawake kiuchumi Dkt.Gwajima alisema
kupitia Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 pamoja na
mkakati wake wa utekelezaji wa mwaka 2005, katika kipindi Cha mwaka
2015 hadi 2020 kiasi cha shilingi Trioni 2.22 zimetolewa Kama mikopo na
kunufaisha vikundi vya wanawake wajasiriamali takribani 490,000 vyenye
wanawake zaidi ya milioni 4.9.
Alisema
mikopo hiyo imetolewa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) kwa
fedha zilizotengwa kupitia vyanzo vya ndani vya Mamlaka za Serikali za
Mitaa kwa kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa
mikopo kwa makundi ya wanawake(4%), vijana (4%) na watu wenye ulemavu
(2%).
No comments:
Post a Comment