HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 15, 2021

BENKI YA STANDARD CHARTERED YAANZISHA SHINDANO LA 'BANK MORE SCORE MORE', MSHINDI KUISHUHUDIA LIVERPOOL

Benki ya Standard Chartered imeanzisha shindano lijulikanalo kwa jina la Bank More Score More, ambapo mshindi atapata fursa ya kutembelea klabu ya Liverpool.

Mbali ya zawadi hiyo, pia benki hiyo itatoa zawadi mbalimbali 350 kwa wateja wao ambao watafanya shughuli za kibenki kidigitali kuanzia kufungua akaunti na matumizi mengine ikiwa mikopo, bima na manunuzi.

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa benki hiyo Ajmair Riaz amesema kuwa mbali ya kutembelea klabu ya Liverpool pia watatoa zawadi kwa wiki ambapo jumla ya washindi 40 watazawadiwa zawadi mbalimbali.

Riaz alisema kuwa mshiriki anatakiwa kutuma neno Bank More kwa njia ya WhatsApp kwenda namba +255714670921 na kuingia moja kwa moja kwenye shindano hilo.

Amesema ili kuweza kushinda, mshindani anatakiwa kupata pointi 200 ambapo haitakuwa na droo ya kupata mshindi.

"Mteja wa kwanza kupata pointi hiyo, atashinda moja kwa moja safari ya kwenda Anfield na kujionea mambo mbalimbali ya klabu hiyo na kujifunza," alisema Riaz.

Alisema kuwa mshindi atapewa nafasi ya kumchagua mtu mmoja wa kuambatana naye ambapo akiwa huku kwa siku tatu atatembelea uwanja wa Anfield, kuona mechi moja na kula chakula cha jioni na mmoja wa magwiji wa klabu ya Liverpool.

Alisema kuwa tiketi ya washindi itaisha muda wake kwa kipindi cha mwaka mmoja na hivyo kumpa fursa ya kuitumia tiketi hiyo pindi atakapo pata nafasi na kuchagua mechi gani atakayopenda kuhudhuria.

Kwa mujibu wa Riaz, shindano hilo litamalizika Juni 11 na kuwaomba wateja wao kushiriki huku akiwahamasisha watu wengine ambao si wateja wao kujiunga kwa kufungua akaunti.


Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa benki hiyo Ajmair Riaz akizungumza na waandishi wa habari  wakati akizungumzia kuhusu shindano lijulikanalo kwa jina la Bank More, Score More ambapo mshindi atapata fursa ya kutembelea klabu ya Liverpool kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered Bi. Juanita Mramba kwenye mkutano  uliofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es Salaam leo.

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa benki hiyo Ajmair Riaz akimsikiliza Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered Bi. Juanita Mramba wakati akizungumzia kuanzishwa kwa  shindano lijulikanalo kwa jina la Bank More, Score More ambapo mshindi atapata fursa ya kutembelea klabu ya Liverpool katika mkutano  uliofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya waandishi wa wakishiriki kupiga danadana mpira katika shindano ambalo washiriki walijipatia zawadi ya jezi.

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa benki hiyo Ajmair Riaz akikabidhi zawadi ya jezi kwa washindi mbalimbali walioshinda kwenye shindano lililofanyika katika mkutano  uliofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es Salaam leo.

 

No comments:

Post a Comment

Pages