HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 20, 2021

Ufaransa yawakumbuka wasichana kwenye kilimohai

Balozi Clavier akiwa na Mkurugenzi wa FCS Trust, Martha Olotu.
Balozi wa Ufaransa Frederic Clavier (katikati) akizungumza na wanaahabaari (hawapo pichani) kuhusu mradi wa kuendelea vijana wa kike na wanawake kwenye kilimohai na endelevu.
Janet Maro Mkurugenzi wa Shirika la SAT.

Na Irene Mark

UBALOZI wa Ufaransa umedhamiria kuboresha maisha ya wasichana na wanawake wa kitanzania waliosahaulika kwa kuwawezesha kwenye sekta ya kilimohai ili kuboresha uchumi wao.

Katika kutimiza dhamira hiyo Ufaransa ikishirikiana na asasi za kiraia imetenga kiasi cha sh. 1,669,561,299 kwaajili kusaidia makundi ya wanawake, wasichana na vijana wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaisha hapa nchini.

Balozi Frederic Clavier alisema hayo jijini Dar es Salaam leo Apili 19.2021 kuwa Ufaransa wametoa fedha hizo kupitia mashirika matatu  yanayofanya kilimohai na endelevu nchini Tanzania.

Aliyataja mashirika hayo kuwa ni FCS Trust, Msichana Initiative, Practical Permaculture Institute of Zanzibar (PPIZ) na Suistanable Agriculture Tanzania (SAT).

“Kwa pamoja tunatekeleza mradi wa miaka miwili tumeuita Empowerment through Agroecology na Permaculture Gape  ambapo ufaransa itaendelea kusaidia eneo la usawa wa kijinsia na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi,” alisema Balozi Clavier.

 Kwa mujibu wa balozi huyo jumla ya wasichana 2,000 sawa na asilimia 90 ya walengwa wa mradi huo watafikiwa na wavulana ni asilimia 10 kutoka mikoa ya Tabora, Dodoma na Zanzibar huku akisisitiza kwamba ni mwendelezo wa mradi wa awali ulioitwa Agroecology.

Akizungumzia mradi huo, Mkurugenzi wa SAT, Janet Maro alisema utaongeza chachu ya wasichana na wanawake kujitegemea zaidi kiuchumi na kuushukuru Ubalozi wa Ufaransa kuona umuhimu wa kuiwezesha jamii hiyo iliyosahaulika hasa kwenye eneo la kilimo.

 “Sisi shughuli yetu ni kilimo hivyo tunaona namna pengo la ushiriki wa wasichana na wanawake katika kilimo lilivyo kubwa... kupitia mradi huu naamini idadi ya wakulima wanawake itaongezeka,” alisema Maro na kuongeza kwamba wanayo masoko ya uhakika ya mazao ya walengwa wa mradi huo.

Mkurugenzi wa Shirika la Msichana Initiative, Rebeca Gyumi alisema wasichana wengi wataakaoshiriki mradi huu ni wale walioaathika na mimba za utotoni hali iliyowatoa kwenye mfumo rasmi wa elimu.

"Mradi huu utakwenda kuwanufaisha vijana na wasichana 1,000 kutoka mikoa ya Tabora Wilaya ya Nzega na Dodoma wilayani Bahi  na kule Zanzibar ni vijana 820  watanufaika na mradi huu moja Kwa moja,” alisema Gyumi.

No comments:

Post a Comment

Pages