HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 14, 2021

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AZURU KABURI LA HAYATI DKT. JOHN M,AGUFULI CHATO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Engineer Gabriel pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali, wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Chato Mkoani Geita leo Mei 14,2021. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akizuru Kaburi la aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati aliposi mama kwa muda Wilayani Chato alipokuwa njiani akielekea Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma kwa ajili ya kufunga Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM za Jimbo la Muhambwe kwa ajili ya UIchaguzi Mdogo wa Kiti cha Ubunge unaotarajiwa kufanyika Jumapili tarehe 16 Mei 2021 kufuatia Kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Hayati Nditye.

No comments:

Post a Comment

Pages