NA HAMIDA RAMADHANI, DODOMA
IMEELEZWA
Kuwa Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto wa kike Unabebwa
na dhana kubwa ya Mfumo dume Umasikini na imani za kishirikiana.
Katika
kuhakikisha wanapunguza na kuondoa kabisa vitendo hivyo vya ukatili
Taasisi ya TGNP Mtandao imekuwa ikijihusisha na Harakati za ukombozi wa
wanawake Kimapinduzi nchini Tanzanian ,Barani Afrika na kwengineko
Duniani.
Taasisi hiyo ya
TGNP Mtandao jana April 14 imetoa mafunzo kwa baadhi ya wabunge
wanawake lengo likiwa nikuwepo kwa elimu juu ya vitendo Vya ukatili
vinavyofanyika lila siku katika jamii ili nawao waende wakapaze sauti
zao Bungeni hasa kipindi hiki cha vikao vya Bunge la Bajeti
vinavyoendelea.
Jackline
Ngoyani msongozi ni Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma ambaye ni moja
Kati ya wabunge wanawake walioshiriki mafunzo ya shirika la (TGNP)
Mtandao juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na
watoto.
Amesema
kupitia mafunzo hayo Wamepata uelewa mpana ambapo sasa, wanakwenda
kuishauri serikali kuweka Mpango Mkakati utakaoenda mpaka katika jamii
inayoishi na wanawake na watoto iliwaweze kuondokana na kutokomeza
kabisa ukatili.
Naye
Mbunge Viti Maalumu kupitia tiketi ya Chama cha Democrasia na Maendeleo
(CHADEMA) Ester Matiko amesema kupitia mafunzo hayo Wameweza kupata
elimu na kujua zaidi takwimu za Mikoa inayoongoza kwa ukatili wa
kijinsia.
"Sasa tumeweza
kutambua serikali inatakiwa kutenga bajeti ya kutosha katika kuhakikisha
mapambano dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto yanaendelea ,"
amesema Matiko.
Kwa
Upande Wake Mwasi Damas Mbunge wa Viti Maalum na ni mwakilishi wa
Vijana Taifa kutoka Mkoa wa Mwanza amesema wamepewa mafunzo ya ukatili
kwa wanawake na watoto lengo likiwa ni kuhakakisha wanapata uelewa juu
ya vitendo Vya ukatili kitakwimu hasa kipindi hiki cha Bunge la bajeti.
"
Tumeweza kubaini ni Mazingira gani ya ukatili yanatokea na na mazingira
gani yamekithiri na hatua kama nchi, serikali na Asasi za kiraia
zimechukua kupunguza tatizo hili,".
Na
kuongeza kuwa"Mafunzo Haya yamekuja kwa kipindi Muafaka kwani wakifika
bungeni tutaisemea agenda hii kwa upanda wake ili fedha itengwe
kulingana na upande wa tatizo hili,"amesema Mwasi.
Aidha
ametoa wito kwa wanaharakati wakupinga ukatili na wabunge wote watumie
nguvu kubwa kulisemea jambo hilo bila kuwasahau Vijana wakike kwani ndio
wameonekana wahanga wakubwa wa tatizo hili.
No comments:
Post a Comment