>Watoto waiombe ushindi Simba kesho
Watoto Yatima wa Kituo cha Umra kilichopo Magomeni wilayani Kinondoni
wakiomba dua pamoja na baadhi ya wawakilishi wa Taasisi ya Simba Jamii
Tanzania Enterprise (SJTE), ili kusaidia Klabu ya Simba kuibuka na
ushindi kwenye mchezo wa marudiano na timu ya Kaizer Chief.
Mwenyekiti wa Taasisi ya
Simba Jamii Tanzania Enterprise (SJTE), Patrick Mwanakatwe akikabidhi
mashuka 30 kwa Muasisi wa Kituo cha Umra Rahma Kishumba (katikati) na
Mlezi wa Kituo hicho Thuwaybaty Ahmada Nassoro (kushoto) wengine ni
watoto.
Muasisi wa Kituo cha Umra kilichopo Magomeni wilayani Kinondoni jijini
Dar, Ramha Kishumba alielezea furaha waliopata kupatiwa msaada waashuka
30 kutoka Simba Jamii Tanzania Enterprise (SJTE), kutosho ni Mwenyekiti
wa SJTE, Patrick Mwanakatwe.
Na Mwandishi Wetu
TAASISI
ya Simba Jamii Tanzania Enterprise (SJTE), imetoa msaada wa mashuka 30
kwa Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Umra kilichopo Magomeni Wilayani
Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Msaada
huo umekabidhiwa na Mwenyekiti wa SJTE, Patrick Mwanakatwe ambaye
aliambata na Mjumbe wa Utendaji Mussa Mongi, Mlezi wa Hassan Mbilili na
Mjumbe wa Kamati ya Habari na Matangazo Suleiman Msuya.
Akizungumza
baada ya kutoa msaada huo Mwenyekiti wa SJTE, Mwanakatwe amesema
dhamira ya taasisi hiyo pamoja na kuishabikia Klabu ya Simba ila
wanahakikisha wanatatua changamoto za jamii kwa kujichangisha kidogo
walichonacho.
Amesema kwa leo wametoa mashuka 30 kwenye kituo cha Umra ambacho kilikuwa kinahitaji hilo.
Mwanakatwe
amesema wamekuwa wakitoa misaada kwa watoto yatima, watu wenye ulemavu
kwa kuwapatia viti lengo likiwa ni kuwapunguzia adha mbalimbali.
"Simba
Jamii Tanzania Enterprise ni taasisi ambayo inahusika na kuishabikia
Klabu ya Simba na huduma za jamii kama kusaidia watoto yatima na wenye
ulemavu wa viungo hivyo leo ni zamu ya Umra tunaendelea kujipanga
kuendelea kusaidia makundi hayo kila kona ya nchi.
Mashuka
30 tuliyotoa hapa ni sehemu ya msaada wetu na tunaendelea kuchangishana
tuweze kuwapatia mahitaji mengine kama magodoro ambayo bado
wanahitaji," amesema.
Mwenyekiti
amesema SJTE ina wanachama kutoka pande zote dunia ikiwemo Japani,
Afrika Kusini, Marekani, Uingereza, Tanzania na kwingineko.
Kwa
upande wake Mjumbe wa Kamati ya Utendaji SJTE, Mongi amewaomba wana
Simba popote walipo duniani kujiunga na taasisi hiyo ili kuweza kusaidia
jamii.
Mongi alisema kwa sasa wapo kwenye mikakati mbalimbali ya kuhakisha SJTE inatangazwa zaidi ili kufikia wana Simba wengi.
Mlezi
wa Simba Jamii, Mbilili alisisitiza kuwa kupitia taasisi hiyo wameweza
kusaidia watu wengi hivyo ni imani yao wataweza kufikia kundi kubwa.
Muasisi
wa Kituo cha Umra, Rahma Kishumba amesema wanashukuru kupata msaada wa
mashuka 30 kutoka Simba Jamii na kuwataka waendelee kusaidia makundi
maalum.
Amesema
Kituo cha Umra kina watoto yatima 117 ambao wamewapata katika maeneo
mbalimbali hivyo kuwataka wadau wengine kuunga mkono juhudi zao za kulea
watoto hao.
"Tunawapongeza
SJTE kwa kuweza kutatua changamoto hii ya mashuka kwani ilikuwa
inatuumiza vichwa ni imani yetu wengine watakuja kutupatia magodoro,"
amesema.
Aidha,
amesema watoto hao yatima waliopo kwenye vituo vyao vinne ambavyo ni
Magomeni, Buza, Mbezi na Vikawe wanahitaji bima ya afya hivyo kuomba
wadau kuwasaidia kwenye eneo hilo.
Kishumba amesema watoto hao yatima wanasoka katika shule mbalimbali jambo ambalo linasaidia kutimiza ndoto zao.
Muasisi
huyo alitumia nafasi hiyo kuiombea ushindi timu ya Simba dhidi ya
Kaizer Chief wanaotarajiwa kuchezwa kesho katika Uwanja wa Benjamin
Mkapa jijini hapa.
Kwa upande wao watoto Yasira Dauda na Abdul Hakimu Nassor wameishukuru SJTE kuwapatia zawadi hizo na kuahidi kuzitunza.
Aidha,
watoto hao wameombea dua timu ya Simba iweze kuibuka na ushindi katika
mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Timu ya Kaizer
Chief.
No comments:
Post a Comment