HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 11, 2021

TCRA: Kila mtu aweke ‘password’ simu yake

 NA HAMIDA RAMADHANI,  MOROGORO

 

MAMALAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema, ujio wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), umeleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya habari bila kusahau haki za msingi za binadamu.

 

Pia, TCRA imewataka wananchi wote, kuhakikisha wanaweka nywila ‘password’ kwenye simu zao na kutokubali kumwonyesha mwenzaa wake kwani ni hatari.

 

 

Hayo yamebainishwa leo Jumanne, tarehe 11 Mei 2021 na Dk. Philip Filikunjombe, Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi na Utekelezaji wa Sheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

 

Alikuwa akiwasilisha mada katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi na wahariri wa habari wa mtandaoni, mkoani Morogoro, iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC).

 

Dk. Filikunjombe amesema, Tehama imeleta mabadiliko katika dunia ya sasa ambapo, dunia imekuwa kijiji kwa kuongeza kwa watumishi wa mtandao huku kasi ya mtandao kuwa ya kasi kubwa.

 

"Ni ukweli usiopingika, tumetoka kwenye matumizi ya kizamani na sasa tupo katika mitandao ya kijamii ambapo huko tunapata habari zetu kwa rahisi na haraka zaidi," amesema Dk. Filikunjombe.

 

Aidha ametoa rai kwa watumishi wa mawasiliano kwanjia ya mtandao kuweka nywila (Password) ikiwemo kwenye simu zao, ili taarifa zao ziwe na usiri ili kuepuka wadukuzi.

 

Amesema, suala la kuweka nywila, haijalishi kama uko kwenye mahusiano ikiwemo ndao kwani Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni za mwaka 2020, zinataka kila mmoja awe na nywila yake mwenyewe pasina mtu mwingine kuijua.

 

Dk. Filikunjombe amesema, kutokana na mjadala wa uwepo wa wadau mbalimbali kutaka maboresho ya kanuni hizo hivyo, TCRA imeanza kupokea maoni ya wadau ili ziweze kuboreshwa.

 

Amesmea, kila mmoja, ajitokeze kutoa maoni yake kwa kuangalia ni eneo gani linahitaji maboresho zaidi yatakayozifanya kanuni hizo kuwa rafiki kwa watumiaji wote.

No comments:

Post a Comment

Pages