Mkuu wa Wilaya mpya ya Bagamoyo wa katikati Zainabu Issa wa katikati akizungumza na wakuu wa idara mbali mbali kutoka Halmashauri za Bagamoyo na Chalinze ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha kwa watumishi ili kujadili Mambo mbali mbali.kulia kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya Bagamoyo Kasilda Mgeni na kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Ramadhani Poss.
NA VICTOR MASANGU,CHALINZE
Mkuu
mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Issa amewataka watumishi na wakuu wa
idara wote kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo kwa
kuzingatia weledi, nidhamu, kutenda haki bila ya kumwonea mtu yoyote kwa
kuzingatia misingi ya Sheria na taratibu.
Kauli
hiyo ameitoa wakati alipofanya ziara yake ya kwanza ya kikazi baada ya
kukabidhiwa rasmi ofisi na kuamua kuwakutanisha wakuu wote wa idara
mbali mbali kutoka halmashauri za Bagamoyo pamoja na Chalinze kwa lengo
la kujadili mipango ya kimaendeleo na changamoto zilizopo.
Mkuu
huyo ambaye aliongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya
Bagamoyo amesema kwamba anamshukuru Sana Rais wa awamu ya sita Mama
Samia Suluhu kuweza kumuamini kimteuwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo na
kuahidi kutoa ushirikiano kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.
''Mm
lengo langu kubwa na kikao hiki ni kukutana na wakuu wa idara ambao
Nina Imani kubwa ndio wataweza kunisaidia katika kutekeleza majukumu
yangu ya kila siku lakini kitu kikubwa ni lazima kuwe na nidhamu katika
suala zima la uwajibikajk ikiwemo pamoja na kutenda haki kwa kila
mmoja,"alisema mkuu huyo.
Pia
alibainisha kuwa lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha
kwamba inawasaidia wananchi kutatua changamoto na kero zao ambazo
zinawakabili katika sekta mbali mbali ikiwemo afya,maji miundonbinu ya
barabara,elimu pamoja na Mambo mengine ya msingi.
Aidha
mkuu huyo kupitia kikao hicho aliwakumbusha wakuu hao wa idara kufanya
kazi kwa bidii na kuhakikisha kwamba wanasimamia vizuri ukusanyaji wa
mapato na kuziba mianya ya upotevu wa fedha ili kutumiza malengo
waliyojiwekea.
Katika
hatua nyingine mkuu huyo wa Wilaya aliwataka watumishi hao kuhakikisha
kwamba waachana kabisa na tabia ya kukaa maofisini na badala yake
wabadilike kwa kuwatembelea wananchi ili kubaini changamoto
zinazowakabili.
Pia
alisema atahakikisha kwamba anashirikiana bega kwa bega na watumishi
wote wa halmashauri za chalinze pamoja na bagamoyo na kuwataka wawe kitu
kimoja na kupeana ushauri katika Mambo mbali.mbali.ikiwemo kuwaletea
wananchi maendeleo.
Kwa
upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni
amemuhakikishia mkuu huyo mpya wa wilaya kumpa sapoti na mshikamano wa
Hali ya juu na kwamba nia ya serikali ya awamu ya sita ni kuwaondolea
wananchi changamoto zinazowakabili.
Naye
mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Ramadhani Posi pamoja na
Mkurugenzi wa halmashauri ya Bagamoyo Fatma Latu wamempongeza mkuu huyo
kwa uamuzi wa kuwakutanisha wakuu wa idara ambao wataweza kuwa kitu
kimoja na kuyatekeleza maagizo yote yaliyotolewa.
No comments:
Post a Comment