NA ASHA MWAKYONDE, DAR ES SALAAM
MATAIFA yenye nguvu yasifumbie macho mapigano yanayoendelea kati ya Palestina na Israeli kwani mauaji yanayotokea ni ya watu wasio na hatia wakiwamo watoto,Wazee, wanawake na watu wanyonge.
Hayo yamesema juzi jijini Dar es Salaam na Sheikh Mkuu wa Mkoa huo Alhad Mussa katika Kongamano la Mshikamano wa Tanzania na Palestina, alisema Israeli inachokifanya ni dhuluma isiyokubalika kwa kila mpenda haki duniani.
Alisema Israeli inachokifanya ndani ya Palestina ni uadui dhidi ya utu na heshima ya nwanadamu na kwamba ni mambo yasiyokubalika na kamwe kuyanyamazia ni haramu si kwa nwislamu, mkiristo na sio kwa mtu yoyote.
" Kunyamazia dhuluma inayotendwa ndani ya Palestina ni haramu kwa sababu utu wa mwanadamu na heshima yake, karama na utukufu wa mwanadamu unachezewa pasipo hatia ni jambo ambalo halikubaliki," alisema Sheikh Alhad.
Sheikh Alhad Aliongeza kuwa ardhi ya Palestina haina shaka na kwamba Mwenyezi Mungu anachelewesha hadi siku ambayo macho yatakapo ya Israeli yakiona adhabu yake.
Aliongeza kuwa Baraza Kuu la Kiislamu Tanzania(BAKWATA), kama chombo cha Waislamu tayari kiongozi mkuu wa chombo hicho Mfuti Sheikh Abubakari Zuberi alitoa tamkp akilaani yale yanayoendelea Palestina juu ya dhuluma.
" Na huu ndio msimamo wa Baraza na ndio msimamo watu wote wanaopenda amani , uzuri wa nchi yetu ya Tanzania ni nchi ambayo imepigania haki na ukombozi wa nchi mbalimbali sio kwa Afrika bali hata nje ya Afrika ,' alisema.
Aidha Sheikh huyo aliwashukuru wandaaji wa Kongamano hilo wakiwamo kikundi cha Happy Hands.
Naye Profesa Issa Shivji alisema kuwa hulka ya Watanzania ni kupambana, kushikamana dhidi ya dhuluma bila kujali walipo, kabila zao uraia wao wamezoea nshikamano hasa uliotokana na mwasisi wake Mwalimu Julius Nyerere.
Alieleza kuwa maelfu ya maelfu ya watu duniani kote wameandamana kupinga na kulaani Waisraeli isipokuwa Watanzania na kwamba ilikuwa ikiongoza Afrika nzima katika kuonyesha mshikamano dhidi ya ukandamizaji.
" Suala la Palestina sio suala la dini mapambano yanayoendelea sio mapambano kati ya Waislamu na wakristo Wapalestina wanapambana na adui mkubwa kwa niaba yetu sote " alisema Prof. Shivji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Mshikamano wa Tanzania na Palestina Abdullah Othuman alisema uhusiano wa Tanzania na Palestina ulianza miaka mingi wakati wa chama kimoja cha Mapinduzi kila kilipokuwa kikifanya mkutano wake mkuu wajumbe wa Palestina ulihudhuria.
" Moja ya nyayo za Mwalimu Nyerere ni kuunga mkono Palestina, kumekuwa na jitihada nyingi za kutuparanganya ili tuondoe msimamo wetu," alisema Othuman.
Aliongeza kuwa Wapalestina walijitoa muhanga kuzisaidia nchi za Afrika Kusini, Angola na Msumbiji walitoa jasho lao, askari ili Uhuru upatikane katika nchi hizo na kwamba Tanzania nayo inajuhudi kubwa ya kuinga Palestina.
Othuman alisema Wapalestina walikuja Tanzania, Hospitali ya Palestina madaktari wakwanza walitoka Palestina walifanya kazi kwa miaka mingi kwa kujitolea bila kulipwa mshahara hivyo huo ni umoja walijitoa kwa ajili ya Watanzania.
No comments:
Post a Comment