Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba akizungumza wakati wa kikao cha Mawaziri wa Sekta mbalimbali kwa ajili ya kujadili, kutoa mapendekezo na maboresho ya Bajeti Kuu ya Serikali kabla ya kuwasilishwa Bungeni, kilichofanyika jijini Dodoma.
NA JOSEPHINE MAJURA, WFM
WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba amekutana na kufanya
mazungumzo na baadhi ya Mawaziri wa Sekta mbalimbali na kuwahakikishia
kuwa maeneo yote ya kipaumbele yatazingatiwa ili kuchochea maendeleo ya
nchi kupitia miradi itakayotekelezwa na Wizara hizo.
Dk.
Nchemba alisema, kuwa lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili na
kupitia maeneo ya vipaumbele kwenye kila sekta ili kuona kama
yamejumuishwa kwenye hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kabla ya kusomwa
Bungeni Jijini Dodoma Juni 10 mwaka huu.
“Nimekutana
na viongozi mbalimbali ili kupunguza mazingira yaliyokuwa yakijitokeza
nyuma kwamba maeneo ya vipaumbele vya Sekta fulani hayajawekwa sawa,”
alisema.
Aliongeza kuwa
maeneo mengi ya vipaumbele yamekuwa yakiwekwa tofauti na matakwa ya
Wizara na Sekta husika hivyo kikao hicho kilikaa ili kubainisha maeneo
ya vipaumbele ambayo hayakujumuishwa kwenye Bajeti Kuu na kuangalia
uwezekano wa kuyajumuisha kama ilivyopendekezwa.
Dk.
Nchemba alieleza kuwa kikao hicho kimejikita katika kujadili
mapendekezo ambayo yaliyopo katika hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan
pamoja na mipango na dira ya maendeleo ya uchumi na Taifa kwa ujumla.
Naye
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Geoffrey
Mwambe amepongeza hatua hiyo kwani italeta tija kwa kuwa kila sekta
imepata nafasi ya kutoa maoni kwa lengo la kuboresha.
“Nampongeza
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu kwa kuitisha kikao hiki ni
utaratibu mzuri sana na unatakiwa kuwa endelevu ili kuleta matokeo
chanya”, alisisitiza Mwambe.
Aliongeza
kuwa katika kikao hicho wameweza kufanya mapitio ya kodi mbalimbali kwa
ajili ya kuzifanyia maboresho ili ziwe rafiki kwa wananchi na kuwafanya
waweze kulipa kwa hiyari.
Aidha
Mwambe alisema, kuwa kodi zikiwa rafiki kwa wawekezaji na
wafanyabiashara wataweza kulipa kwa wakati na kodi hizo zitaisaidia
Serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kikao
hicho cha Mawaziri wa Sekta kimefanyika katika ofisi ya Waziri wa Fedha
na Mipango Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Mawaziri mbalimbali wa
Wizara 9 ikiwemo Viwanda na Biashara, Kilimo, Mifugo, Maliasili na
Utalii, Afya, Ardhi, TAMISEMI, Uwekezaji na Wizara ya Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment