HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 30, 2021

Mwakabuku: kwa mara ya kwanza tumealika kampuni za mipango miji na za upimaji


Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam


WIZARA ya Ardhi Nyumbai na Maendeleo ya Makazi imealika baadhi ya kamupuni za mipango miji na za upimaji ili kuonyesha uaminifu wa Wizara hiyo kwa wananchi.

Akizungumzia jijini Dar es Salaam katika Maonyesho ya  45  Biashara ya Kimataifa  ya Dar es Salaam.(DITF), Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Ardhi Lusajo Mwakabuku amesema urasimishaji haifanyi Wizara kuna kampuni ambazo zimesajiliwa na Wizara hiyo.

Mwakabuku amesema kuwa lengo la kusajili kamupuni hizo ni kuwasaidia wananchi urahisi wa kupata nyaraka zao muhimu za viwanja.

Amefafanua kuwa  rasilimali zao hazitoshi kuzunguka nchi nzima ndio maana kampuni hizo zikasajiliwa ili zifanye kazi ya kuwasaidia wananchi wenye uhitaji.

" Kuna kampuni za upangaji  ambazo zinafanya kazi ya upangaji na kuna za upimaji ambazo zinafanya kazi ya upimaji yote haya yamesajiliwa na Wizara,: ameongeza.

"Mwaka huu tumejitahidi kualika baadhi ya kamupuni zipo hapo katika jengo letu la Maonyeshoya kwa ajili ya kutangaza kazi zao na kutoa uthibitisho kuwa wanafanya kazi hizo na kwa kutumia utaratibu gani,"ameeleza Mwakabuku.

Ameongeza kuwa hata mwananchi akienda  jengo la ardhi lililopo katika maonyesho hayo  kama alikuwa na wasi wasi na urasimishaji wanaweza kumuunganisha na kamupuni hizo wakamuondoa hofu  kuthibitisha baadhi ya kazi ambazo wamezifanya.

No comments:

Post a Comment

Pages