Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Othman Masoud Othman,
akiwasili kisiwani Zanzibar leo Juni 23, 2021 akitokea jijini
Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amerejea nyumbani kisiwani Zanzibar Leo Juni 23, 2021 akitokea jijini Dar es Salaam.
Makamu Hugo wa Kwanza wa Rais alikuwa jijini Dar es Salaam alikokuwa kwa shughuli maalum za kichama tangu Juni 19, 2021.
Akiwa jijini Dar es Salaam, Othman ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo alihudhuria kikao cha Kamati kuu pamoja na kufanya ziara ya kuwajulia hali wagonjwa na wananchi wenye matatizo mbali mbali sambamba na kuzungumza na wanachama na viongozi wa chama hicho ngazi ya taifa, mkoa, majimbo na Kata ya Mbagala Kuu.
No comments:
Post a Comment