HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 20, 2021

‘Toeni maoni tupate bodi bora tuondoe makanjanja wa elimu’




 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akifungua mkutano wa wadau wa Elimu kuhusu Bodi ya Kitaalamu ya Walimu jijini Dar es Salaam leo Juni 19, 2021.


Wadau wakiwa katika mkutano wa wadau wa Elimu kuhusu Bodi ya Kitaalamu ya Walimu jijini Dar es Salaam leo Juni 19, 2021. 

Mdau akitoa maoni yake katika mkutano huo.
 

Na Irene Mark

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewataka washiriki wa mkutano wa wadau wadau kujadili Sheria na Kanuni za uanzishwaji wa Bodi ya Kitaalamu ya Walimu kufanya hivyo kwa kuzingatia mazingira ya walimu na kuondoa makanjanja kwenye tasnia hiyo.

Akiongoza mkutano huo uliofanyika leo Juni 19.2021 jijini Dar es Salaam, waziri huyo alisema kuanza kwa bodi hiyo kutaondoa makanjanja wa elimu na kuongeza hadhi na ubora fani hiyo hapa nchini.

Alisema mwaka 2009 serikali ilipokea maombi ya walimu wakitaka iwepo bodi itakayosimamia haki, stahili na hadhi za walimu hapa nchini.

“Serikali iko tayari kupokea maoni na mapendekezo yanayotolewa na wadau juu ya nini kifanyike ili kuboresha sheria na kanuni zinazounda Bodi ya Kitaalamu ya Walimu Tanzania... ndio maana leo tuko hapa na kazi hii naamini tutaifanya kwa weledi.

Kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, mwaka 2018 Bunge lilipitisha muswada wa sheria ya kuunda Bodi ya Kitaalamu ya Walimu ya Tanzania, ambapo Wizara ya Elimu ilitunga kanuni za kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo baada ya kusainiwa kwa sheria.

Amesema baada ya kutungwa kwa kanuni za bodi hiyo, Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kilielezea kutoridhishwa na baadhi ya vipengele vya kanuni hizo, hivyo wizara imeona ni vema kuwashirikisha wadau ili kusikikiza maoni yao na kuondoa changamoto katika utekelezaji wa majukumu ya Bodi ya Kitaaluma ya Walimu Tanzania.

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Leah Ulaya alisema watatumia fursa hiyo adhimu kutoa maoni yenye tija kwa maendeleo endelevu ya elimu.

“Tuliiomba bodi hii tukiamini itatusaidia sana na serikali imepokea maombi yetu licha ya muda kupita lakini imeyafanyia kazi tunaishukiru sana kwa kuwa imetushirikisha kwenye kuanza kwa kitu tulichokiomba,” amesema Ulaya.
 

No comments:

Post a Comment

Pages