Dk. Consolatha Ishebabi (kushoto mbele) kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara akiwasilisha rasimu kwa wadau wa sekta binafsi kabla ya kuanza kwa majadiliano kwa washiriki. |
Warsha ya wadau wa sekta binafsi pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara kujadili mapitio ya rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo ikiendelea leo jijini Dar es Salaam. |
Warsha ya wadau wa sekta binafsi pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara kujadili mapitio ya rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo ikiendelea leo jijini Dar es Salaam. |
WADAU wa sekta binafsi pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara leo wamekutana jijini Dar es Salaam kujadili mapitio ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo huku ikiwa ni mchakato wa maboresho wa sera hiyo muhimu nchini.
Akizungumza na wadau hao
wakati akizindua mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na
Biashara, Dk. Hashir Abadallah amewataka washiriki hao kupitia kwa makini rasimu
hiyo na kutoa mapendekezo yatakayoiboresha zaidi ili kupata sera inayokidhi
mahitaji na hasa katika dunia ya leo.
Dk. Abdallah amewataka
wajumbe waliopata fursa hiyo kuhakikisha wanatoa maoni bila kujipendelea wao
pekee, bali kwa kuzingatia maslahi ya wajasiliamali wote.
Aliwataka kutambua kuwa Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na
Biashara Ndogo’ nchini inayoandaliwa ibabeba wajasiriamali zaidi
ya milioni 4.5 hivyo inaitaji umakini katika maandalizi yake ili kuja na
suluhisho ya changamoto nyingi kwa wajasiliamali.
“Kwa bahati nzuri zaidi, sekta hii ndio inayobeba takribani
asilimia 98 ya viwanda vyote nchini. Hii ni faraja kwa kuwa malighafi za nchi
yetu hasa za wakulima zinapata masoko katika viwanda hivyo hasa ikizingatiwa
viwanda vya sekta hii vimesambaa nchini kote na vingi vikijihusisha katika
uongezaji thamani hasa wa mazao ya kilimo,” alisema.
Aidha
Naibu Katibu Mkuu alibainisha kuwa Serikali inatambua na kuthamini umuhimu wa
sekta binafsi nchini hususan thamani ya uendelezaji wajasiriamali katika
kuendeleza shughuli za uchumi wa nchi.
Alisema sera za nchi zimeweka bayana
nafasi na jukumu la sekta binafsi katika shughuli za moja kwa moja za
uzalishaji na kufanya biashara.
“Dira ya Taifa 2025, Ilani ya CCM ya
2020 -2025 na Mpango wa Tatu wa Miaka Mitano wa Maendeleo, pamoja na mambo
mengine zinatilia mkazo kuishirikisha ipasavyo sekta binafsi katika kuendeleza
au kukuza jasiriamali katika kukuza biashara zinazochochea mauzo ya nje ili
kuleta uwiano wa maendeleo,” alisema.
No comments:
Post a Comment