HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 22, 2021

WAKAZI MSAMALA NA MWENGEMSHINDO SONGEA WAOMBA KUJENGEWA BARABARA YA LAMI

 

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Maiko Mbano.


NA STEPHANO MANGO, SONGEA

 

WANANCHI wa Kata ya Msamala na Mwengemshindo katika Halmashauri ya Manspaa ya Songea mkoani Ruvuma wameitaka Serikali kuona umuhimu wa kutengeneza barabara kwa kiwango cha lami kutoka Mauki kupitia Mkuzo kuelekea Mwengemshindo kutokana na barabara hiyo kuwa kiungo muhimu katika shughuli za uchumi.

 

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana walisema kuwa barabara hiyo ina hudumia watu wengi na pia inapitisha magari makubwa ambayo yanabeba mchanga kutoka Mwengemshindo, kokoto kutoka Luhira kati na matofari kutoka Mitendewawa

 

Mozes Nyirenda ambaye ni mkazi wa Msamala alisema kuwa kwa muda mrefu barabara hiyo imekuwa kero kubwa sana kwa wananchi kutokana na ubovu wake kutokana na ubize wa shughuli za uzalishaji mali unaofanywa na wananchi ambao wanaitumia barabara hiyo

 

Nyirenda alisema kuwa kwa kuwa barabara hiyo imekuwa ikitengenezwa kwa kiwango cha vumbi na muda mchache imekuwa ikiharibika, hivyo ni muhimu sasa Serikali ikaweka lami ili kuondsokana na kero hiyo ya kutengeneza mara kwa mara

 

Alisema kuwa mara nyingi barabara hiyo imekuwa ikikwanguliwa bila kuwekwa mifereji na kuwekwa udongo ambao haufai na kusababisha kutokudumu kwa muda mrefu hali ambayo inaendelea kuwa kero kwa wananchi

 

Alisema kuwa kutokana na ubovu wa barabara hiyomajira ya kiangazi na kifuku kumekuwa na adha kubwa ya usafiri kwa abiria na hasa watoto ambao wanasoma katika shule za Msingi na Sekondari kwani wenye magari ya abiria wamekuwa wakiyapaki magari yao kuhofia kuyaaribu kutokana na mashimo makubwa katika barabara hiyo

 

Naye Godluck Nyoni alisema kuwa Serikali inapaswa kuondoa kero hiyo kwani barabara hiyo inatumiwa na wananchi wa kata nne na pale ambapo usafiri unakosekana ni hatari sana kwa shughuli za kielimu na kiuchumi

 

Nyoni alisema kuwa barabara hiyo ni kiungo muhimu sana kwasababu ndio njia kuu ambayo inaelekea mjini kutoka mashambani yaani mazao kutoka Chandarua,Kitulo, Ngorohora, na Mwengemshindo yanapitia barabara hiyo

 

Kwa upande wake Eng Niko Danda alisema kuwa barabara hiyo imekuwa ikitengewa fedha za matengenezo madogo madogo mara kwa mara na kwamba ipo kwenye mpango wa ujenzi wa kiwango cha Changarawe.

 

Akizungumzia kero hiyo Diwani wa Kata ya Msamala ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Maiko Mbano alisema kuwa barabara hiyo ni kubwa na inatumiwa na wananchi wengi sana

 

Mbano alisema kwa kipindi kirefu imekuwa ni kero na kwamba kwasasa Tarura wamejipanga kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha Changarawe ili kuweza kuinusuru barabara hiyo na kwamba mipango ya baadae ni kuijenga kwa kiwango cha lami

 

Alisema wananchi waendelee kuwa wavumilivu na kwamba mipango ya kuijenga kwa lami barabara hiyo ipo na kwamba tayari wameanza kuratibu kikao cha pamoja na baina ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) na Mamlaka ya Usimamizi wa Barabara Tanzania (TANROADS)  ili kutafuta majawabu ya pamoja ya kutatua changamoto hiyo kwasababu kunasehemu barabara hiyo inaingia kwenye barabara ya Mtwara Corrido.

No comments:

Post a Comment

Pages