Mwandishi Wetu
CHAMA
cha ACT Wazalendo kimeelezwa kushtushwa na ajali ya moto iliyoteketeza
Soko Kuu la Kariakoo Jumamosi Julai 9, 2021 na kusababisha taharuki,
majonzi na hasara kubwa kwa wafanyabiashara wa soko hilo.
Taarifa
ya chama hicho kwa umma iliyotolewa na Naibu Katibu Mwenezi wake,
Janeth Rithe leo Julai 13, 2021 imesema chama hicho kinatoa pole kwa
wafanyabiashara wote wa soko hilo waliopoteza mali zao na kuwasababishia
umaskini ambao hawakuutarajia.
"Sisi
ACT Wazalendo tukiwa sehemu ya Jamii ya Watanzania tunatoa ushauri kwa
mamlaka za Serikali kuamka sasa na kupitia maamuzi yao kuhusu mazingira
na miundombinu yote inayolizunguka Soko la Kariakoo."
"Mathalani,
taarifa ya Jeshi la Zimamoto kwamba soko hilo halina Kituo au (vioski)
maalum vya maji kwa ajili ya dharura kama hizo linashtua sana." amesema
Rithe.
Mbali na hilo ACT
Wazalendo kimesema kitendo cha mamlaka za Serikali kuruhusu ujenzi
holela wa maduka yaliyopachikwa pembeni kwa kulizunguka Soko la Kariakoo
tofauti kabisa na asili ya muundo wa soko hilo unaweza pia kuwa chanzo
cha moto huo
na hata kusababisha ugumu kwa vikosi vya Zimamoto na Uokoaji kufanyakazi zao kwa ufanisi.
"Aidha
tumeshangazwa mno na uwezo usioridhisha wa Kikosi cha Zimamoto na
Uokoaji ambacho hakipo umbali mrefu na Soko la Kariakoo lakini
kilishindwa kudhibiti moto huo usisababishe madhara makubwa kama
ilivyotokea."amesema.
Aidha
Rithe ameishauri Serikali kuamua sasa kuweka miundombinu mizuri naya
kisasa kwenye masoko, stendi za mabasi na maeneo yote yenye msongamano
wa watu ili kuepuka kusababisha hasara na pesa za walipakodi kuteketea
kwa mambo yanayoweza kuepukika.
No comments:
Post a Comment