HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 14, 2021

VYUO VIKUU VYATAKIWA KUFANYA TAFITI KWENYE VIWANDA

 Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

MAKAMU wa Pili wa  Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah, ameviagiza vyuo vikuu nchini kufanya utafiti wa mahitaji halisi kwenye viwanda nchini ili vitumike kukuza uchumi.


Alisema kufanya tathmini kwenye viwanda hivyo kutasaidia pia kufahamu mahitaji halisi aya rasilimali watu na pia itasaidia kupunguza tatizo la ajira.

Pia, meziagiza taasisi zinazosimamia wafanyabiashara na wazalishaji kutoka pande zote za muungano kutatua changamoto ambazo bado zinaonekana ni kikwazo kwa biashara.

Abudullah alitoa agizo hilo jana wakati akifunga Maonyesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara Dar és Salam aliyoanza rasmi Juni 28 mwaka huu.

Alisema kutatua changamoto hizo  kutasaidia wafanyabiashara na wazalishaji kushindana katika soko la ndani na nje ya nchi.

Pia aliagiza kuhakikisha kwamba bidhaa za ndani na vifungashio vinaboreshwa zaidi kukidhi soko la kimataifa.

Alitoa wito kwa wazalishaji wa Tanzania kupeleka bidhaa zao  nje ya nchi.

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Omary Said Shaaban, alisema maonyesho ya mwaka huu yameakisi lengo la kuyafanya kuwa ya kimataifa.

Alisema maonyesho hayo yamekuwa sehemu kubwa ya kujitangaza na kubadilishana uzoefu katika maeneo yao kufanyia kazi.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo, alisema mpaka jana asubuhi waliokiwa wametembelea maonyesho hayo mwaka huu walikuwa ni 227,000.

Alisema bidhaa zilizoongoza kuuzwa ni za kitanzania ambazo ni mazaó ya kilimo, korosho, chai na kahawa.

Pia alisema katika maonyesho hayo, bidhaa za ngozi nazo zimeuzwa kwa kiwango kikubwa.

Profesa Kitila alisema katika maonyesho hayo, hudumambalimbali za afya zilitolewa ikiwamo za matibabu ya moyo, macho na kuhudumia pia wagonjwa wa dharula.

Alisema mwakani wamepanga maonyesho hayo yawe makubwa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Pages