Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho, Francis Alfred, akizungumza na waandishi wa habari katika banda la bodi hiyo.
Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
BODI ya Korosho imesema ina mpango wa kuongeza uzalishaji kutoka wastani wa tani 300,000 hadi kufikia tani 700,000 ifikapo mwaka 2025/26.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana ndani ya banda la bodi hiyo kwenye Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maalufu Sabasaba aliyoanza Juni 28 mwaka huu yenye kauli mbiu ' Uchumu wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu'.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Francis Alfred amesema wanaifikiria kwenda kuongeza uzalishaji wa korosho ghafi na kwamba wanataka pia kuhamasisha uongezaji wa thamani katika zao hilo la korosho.
"Lngo letu la kushiriki maonyesho hayo ni kuonyesha wadau na washiriki wa maonyesho hayo ya sabasaba kwamba zipo fursa nyingi za uongezaji wa thamani katika zao hili,”ameongeza.
“Cha kwanza ni katika kuongeza ubanguaji, sasa hivi tunabangua wastani wa asilimia 10 ya korosho zetu zote ambazo tunazizalisha , kwa hiyo tunataka kuongeza ubanguaji ufike asilimia 60 kufikia mwaka 2025/26, kwa hiyo hapa tunaonyesha wadau mbalimbali fursa zilizopo kwenye upande wa ubanguaji wa korosho , tuuze zaidi korosho iliyoanguliwa kuliko kuuza korosho ghafi na tukifanya hivyo tutakuwa na uhakika zaidi wa soko la korosho,”amesema Alfred.
Amesema kufanya hivyo kutaongeza uhakika zaidi wa soko la korosho kwa sababu wataweza kuuza katika nchi nyingi kuliko ilivyo sasa hivi ambapo wanategemea soko kutoka katika nchi mbili ambazo ni India na Vietnam.
Kaimu Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa wanataka kupanua wigo wa soko kwa kubangua korosho na kuziuza katika nchi za Marekani, Bara la Ulaya, Mashariki ya Kati, China, Uarabuni, Bara la Afrika.
“Lakini pia tunataka kupanua soko la ndani, sasa kwa walaji wa soko korosho la hapa nchini ambalo bado ni dogo sana kwa sababu ya bei, lakini tukiongeza ubanguaji bei zitashuka na ulaji wa korosho nchini utaongezeka,”ameeleza.
Amesema Julai saba(7) mwaka huu watakuwa na siku maalum ya kuwagaiwa korosho bure washiriki wa maonyesho hayo na kwamba lengo likiwa ni kuhamasisha watu wale korosho ili wapate manufaa ya zao hilo.
“Tunataka zao la korosho liwe na manufaa zaidi katika jamii kwa maana kwamba na njia pekee ni wadau mbalimbali kushiriki katika mnyororo thamani wa zao hili kuanzia shambani na uongezaji wa thamani wa bidhaa mbalimbali zinazotokana na zao hilo," anesema.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Udhibiti Ubora wa bodi hiyo
Domina Mkangara,ameseema wameshiriki katika maonyesho hayo kuonyesha Watanzania fursa mbalimbali zilizopo katika zao hilo.
Mkangara ameseema ni vema Watanzania kupendelea kura korosho kwa kuwa ina manufaa kubwa na kwamba zipo bidhaa mbalimbali watajioneza katika banda hilo ili kufahamu eneo la kuwekeza katika zao hilo.
No comments:
Post a Comment