Baadhi ya wateja waliotembelea Banda la TTCL leo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam wakipatiwa huduma mbalimbali. |
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limewakaribisha wananchi wanaotembelea Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam kutembelea Banda la TTCL kujipatia bidhaa na huduma mbalimbali za shirika hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ndani ya Banda namba 65 la TTCL, Meneja wa Banda la TTCL, Bw. Ramadhani Mshana alisema huduma zinazopatikana ndani ya banda la TTCL ni pamoja na kutoa bure line za simu (Simcard) kwa wateja zikiwa na MBs na dk na sms za kutosha kwa matumizi ya wiki nzima bure.
Alisema ili mteja anufaike na huduma hizo anatakiwa kuwa na kitambulisho cha taifa kwa kusajilia. Alizitaka taasisi binafsi na za Umma zinazohitaji kupatiwa huduma za call center na huduma za mkutano kwa njia ya Video (Video conference) kutembelea banda la TTCL kupata suluhisho ya huduma hizo, pamoja na huduma za kuunganisha wateja wa simu na intaneti kwa njia za Copper, Fiber, na Microwaves (Radio).
"Bidhaa zingine zinazopatikana ndani ya banda letu ni pamoja na Vifaa vya 'wireless internet' kama MiFi, Router, Dongle, Wingle Simu za mezani za Wireless maarufu kama FWT, Router mpya ya kisasa kabisa ambayo ina uwezo wa kuunganishwa na simu ya mezani (kichwa cha simu). Hii ni kwa matumizi ya ofisi na majumbani Kadi za malipo N-card, alisema Meneja wa Banda la TTCL, Bw. Ramadhani Mshana.
Baadhi ya wateja waliotembelea Banda la TTCL leo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam wakipatiwa huduma mbalimbali. |
Kushoto ni watoa huduma wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakihudumia wananchi waliotembelea Banda la TTCL leo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. |
No comments:
Post a Comment