HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 22, 2021

Anna Mghwira afariki dunia

 

Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa huzuni na masikito makubwa taarifa za kifo cha Mama Anna Elisha Mghwira kilichotokea leo 22 Julai, 2021 katika hospitali ya Mount Meru, Arusha alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mama Anna Mghwira alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa ACT Wazalendo mara baada ya Chama kupata usajili wa kudumu kuanzia mwaka 2015 hadi 2017. Mbali ya kukitumikia Chama katika nafasi hiyo, Mama Anna aliteuliwa na Chama kigombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Taifa limempoteza kiongozi mwenye upeo na uwezo mkubwa wa masuala mbalimbali. Pamoja na kwamba Mama Mghwira hakuwa mwanachama wala kiongozi katika Chama chetu mpaka umauti unamkuta, historia yake kwa Chama chetu iliacha alama zisizofutika. Chama kinautambua mchango na uongozi wake alioutoa wakati alipokuwa Mwenyekiti wake wa Taifa. Tutaukumbuka na kuuenzi daima.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.

No comments:

Post a Comment

Pages