HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 15, 2021

Chuo Kikuu Mzumbe kuanzisha ALUMNI Taifa




Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe (Taaluma), Prof. Ganka Nyamsogoro ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao cha UMOJA wa Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe ‘Alumni’ Kanda ya Dar es Salaam, akizungumza katika kikao cha kupitia rasimu ya katiba ALUMNI Taifa, ukiwa na lengo la kuboresha taaluma ya wahitimu wa chuo hicho wawapo eneo la kazi.
 Mkuu wa Ndaki ya Dar es Salaam Prof. Honest Ngowi, akizungumza katika kikao hicho.
Kuchangia mada.

Baadhi ya wanachama wa ALUMNI Mkoa wa Dar es Salaam.

Mwanachama wa ALUMNI mkoa wa Dar es Salaam, Deogratius Kilawe, akijitambulisha katika kikao hicho.

Mratibu wa Umoja wa Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe (ALUMNI) ambaye pia ni Mhadhiri Chuo Kikuu Mzumbe, Dk. Daudi Pascal Ndaki, akizungumza katika kikao hicho.
Picha ya kumbukumbu.
 


Na Mwandishi Wetu

 

UMOJA wa Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe ‘Alumni’ Kanda ya Dar es Salaam umekutana kupitia rasimu ya katiba ya ALUMNI Taifa, ukiwa na lengo la kuboresha taaluma ya wahitimu wa Chuo hicho wawapo eneo la kazi.

Kikao hicho kilifanyika jana, Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam ambapo wajumbe wa kikao hicho walijadiliana namna bora ya kuboresha taaluma yao na taaluma ya wanafunzi waliopo chuoni.

Akizungumza na Habari Mseto Mwenyekiti wa kikao hicho Prof. Ganka Nyamsogoro ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, alisema Lengo lilikuwa kujadiliana namna bora ya kushirikiana kwa wahitimu wa Mzumbe ili Chuo na wahitimu waweze kufanya kazi kwa pamoja.

“Tulikuwa na kikao chetu cha kwanza cha wahitimu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe pamoja na IDM Alumni, lengo ilikuwa ni kujadiliana namna bora ya kushirikiana pamoja ili Chuo pamoja na wahitimu walioko eneo la kazi waweze kufanya kazi vizuri.

“Tumekuwa na wahitimu wengi wa Chuo kama Taasisi kwa miaka mingi, wengi wamefika mbali lakini hatuoni mchango wao ukirudi kwenye taasisi yetu, tunatamani tuweze kuwatumia kuboresha taaluma yetu lakini pia kuboresha ubora wa wahitimu wetu. alisema Prof Nyamsogoro na kuongeza kuwa.

“Pamoja na hayo tumezungumza juu ya mikakati ya kuwa na Chama chetu cha ALUMNI TAIFA ambayo itatuunganisha pamoja, lakini pia mikakati ya kuhakikisha kwamba Chuo pamoja na mahala pa kazi vinaenda pamoja ikiwa ni pamoja na nafasi ya wanafunzi kufanya mazoezi kwa vitendo ‘Field Attachment’, wahitimu kufanya mazoezi ‘internship’ pamoja na walimu wetu kufanya mazoezi. Lakini pia kupata wataalamu kutoka eneo la kazi kuja chuoni kutoa uzoefu wao.

“Lengo ni kufanya wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe waendelee kuwa bora zaidi wakipata radha na vionjo vya mahala pa kazi wakiwa bado shule na hivyo kuongeza kitu cha ziada wanapokuwa eneo la kazi.

“Tumekusudia na tutapita katika kanda mbalimbali, tunakikao kingine Zanzibar kesho (leo), wiki ijayo tutakuwa na kikao Mwanza, tutapita Dodoma, Mbeya, Arusha, Katavi na sehemu nyingine tupate mawazo ya namna ya kuboresha kabla ya kukutana Novemba 24.

 

“Lakini Novemba 23 tutakuwa na Alumni Marathon kwa ajili ya kutuweka pamoja Chuo Kikuu mzumbe na wahitimu wetu kuelekea kwenye mkutano wa Baraza hiyo Novemba 24.” Alisema Prof. Nyamsogoro.

Kwa upande wa waajumbe wa kikao hicho waamepongeza dhamira ya Chuo kuwakutanisha na lengo la kuboresha taaluma zao sehemu ya kazi pamoja na waanafunzi walioko chuoni.

Wakili Obed Kasambala ambaye ni Mwenyekiti wa Alumni Dar es Salaam, alisema jambo hilo limekuja wakati sahihi licha ya kuchelewa lakini litaongeza ufanisi wa waahitimu sehemu za kazi.

“Ni wakati sahihi ila tumechelewa sana, lakini wanasema bora uchelewe lakini ufike. Kwa hapa tuliopoanza ni sehemu nzuri, kinachohitajika tu ni umoja wetu kuwa pamoja na hili lisiwe tu kwetu sisi bali hata kwa watu wengine waweze kujifunza hiki kitu ambacho tunakifanya kwa sababu lengo kuu ni kusaidiana sisi wenyewe kwa wenyewe na kuweza kutambua mwenzetu yuko wapi  anafanya kitu gani, hata kama ana jambo basi tunaweza kumsaidia ili kufikia malengo yake ambayo yeye kajiwekea.

“Nitoe rai kwa wahitimu wengine wa Mzumbe wasikiapo jambo hili wasisite  kuonyesha ushurikiano ili tuweze kufikia malengo yetu.” Alisema Wakili Msomi Kasambala

Nae Deogratius Kilawe alisema umoja huo ni sehemu  muhimu ambayo Chuo Kikuu cha Mzumbe kinapaswa kujivunia kuwa nacho ili kuweza kujitathimini katika mambo mbalimbali.

“Tumekuwa na kikao kizuri kwa ajili ya kuaninzisha Alumni ya Mzumbe Taifa, ambapo tumezungumzia Katiba, Sera ya Tuzo za Alumni pamoja na mambo mengine. Nadhani ni kitu muhimu Mzumbe kuwa na Alumni, kwani ni sehemu ambayo itakuwa inatoa ushauri katika mambo mbalimbali hivyo ni sehemu amabyo Mzumbe itakuwa inajivunia kwani ni mazao yake.

“Pamoja na mapitio haya ya Mswaada wa katiba lakini pia tutakutana Novemba kama Baraza ili kupitisha na kujadili kwa pamoja jinsi gani tunaendelea kuwa kivutio cha vijana wengi kuja kusoma Mzumbe.”

Kwa upande wa Mratibu wa Umoja wa Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe ‘Alumni’ Dkt Daudi Ndaki alisema kikao hicho kimekuwa na mafanikio makubwa kwa wajumbe kujitokeza kwa ajili ya kutoa maoni ya kuwezesha umoja wao kusonga mbele.

“Kikao hiki kilikuwa kikao cha kwanza ambacho kimekuwa na mafanikio makubwa kwa wajumbe kujitokeza kutoa maoni yao kwa ajili ya kuhakikisha umoja wetu unasonga mbele. Kama mnavyofahamu umoja huu ni mkubwa, kuna watu wengi waamepitia Chuo Kikuu Mzumbe kuanzia IDM mpaka Chuo Kikuu Mzumbe.

“Tumeweza kufanikiwa kwa leo (jana) kupata idadi ya Alumni ambao wameweza kutoa maoni kwenye namna bora ya kuweza kuboresha ushirikiano wetu, pamoja na mambo mengine yaliyozungumziwa wana Alumni wameonyesha hamasa kubwa sana ya kuunga mkono huu umoja na tunaamini umoja wa wahitimu wa Chuo Kiku Mzumbe ni Umoja  mkubwa.

“Tunawashauri wale wote ambao hawajajiunga na umoja huu kwa kusajili majina yao kwenye mtandao wetu ambao tulishautoa kwenye makundi yetu basi wajiunge kwa Ada ya elfu 50,000. Kwa mwaka.

Alisema utaratibu huo wa Ada utamfanya mwana Alumni kuwa hai lakini pia aliongeza kuwa mchakato wa katiba umekamilika ni suala la kukusanya maoni ya mwisho kabla ya kikao cha Baraza cha kupitisha katiba hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages