HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 14, 2021

TET YAELEZA SABABU ZA KUSITISHWA SOMO LA HISTORIA


Na Mwandishi Wetu


TAASISI ya  elimu  Tanzania (TET)  imetolea  ufafanuzi  ya kusitishwa  somo  la  historia  kutokana  na  sababu  zinazoeleza  kuwa  vitabu  vya  kiada  viliandikwa  kama  program  za  kusifu  watawala.

Taarifa  iliyotolewa  na  Mkurgenzi  Mkuu  wa  Taasisi ya  Elimu Tanzania (TET)  Dkt. Aneth  Komba  imetolea  ufafanizi  kuwa  hakuna  somo  lolote  lililowahi kuanzishwa  lenye  lengo la kufundisha  historia  ya kumtukuza  kiongozi  yeyote  nchini.

Taarifa  ya  Dkt. Aneth Komba  inasema TET iliandaa maudhui  ya somo la Historia ya Tanzania  mnamo  Machi, 2021  na ilikuwa  bado  haijaanza  kuchapa vitabu  na  hivyo  mwezi  Aprili 2021 ilipokea maelekezo  kutoka  wizara  ya Elimu,Sayansi  na Teknolojia  kuhusu kufanyia  mapitio ya mitaala ya  elimu kwa  ngazi  zote ili  kuhakikisha kuwa  elimu inayotolewa  inatoa  ujuzi wa  kuwawezesha wahitimu kujiajiri,kuajiriwa na kumudu maisha  yao  ya  kila siku.

TET  imeanza  zoezi  la kukusanya maoni  ya wadau  kwa kupitia njia mbalimbali, ikiwemo kufanya mikutano  na wadau  wa Elimu  hatua itakayowezesha  kufanya  mabadiliko  ya  mitaala kwa  kuzingatia mahitaji yote  muhimu ikiwa  ni  pamoja  na kuweka  msisitizo  kwenye  historia  ya  Tanzania.

Aidha  Taasisi  ya Elimu Tanzania  imewaomba  wananchi wote  kushiriki  vema  katika  zoezi linaloendelea  la  kutoa  maoni yatakayosaidia  kuboresha  mitaala  ya ngazi ya Elimu ya  Awali,Msingi,Sekondari  na  Elimu  ya Ualimu kupitia  tovuti ya TET.

No comments:

Post a Comment

Pages