Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Mwanasiasa,
Edna Sunga amezindua kipindi cha Tv cha Edna Sunga Connection chenye
lengo la kuisaidia jamii yenye matatizo mbalimbali pamoja na kuwasaidia
watu wenye vipaji ambao hawajapata nafasi ya kusikika wala kuonekana.
Akizindua
kipindi hicho leo jijini Dar es Salaam Edna amesema ameamua kuanzisha
kipindi hicho kutokana na kupitia changamoto mbalimbali za kimaisha na
kwamba jamii itapata fursa ya kuonyesha viapaji ilivyonavyo na kusaidiwa
kutatua matataizo yanayoikabili.
Amebainisha
kuwa kipindi hicho kwa sasa kimeanza kuonyeshwa katika EDNA SUNGA TV
kupitia cheneli ya Youtube na kwamba kitasaidia kuona vipaji vingi na
vikubwa visiotumika au kunyimwa nafasi.
" Watu
wengi wananifahamu kama mwanasiasa hawajui nilianzia niliingia katika
siasa nikitokea kanisani kwa lengo moja tu Mungu anitumie kulisaidia
taifa langu na watu wake kwa vile wanavyotakiwa kuwa na haki," amesema
Edna.
Amesisitiza kuwa kuna vipaji vingi katika
jamii ambavyo havijapewa nafasi wakiwemo wasanii wa maigizo,
wanamitindo, Mamc, waimbaji wa nyimbo za dini pamoja na wanamuziki hivyo
kupitia kipindi hicho watapata fursa ya kujulikana kwa kuunganishwa
katika sehemu husika.
Ameongeza kuwa kipindi
hicho kitatoa usaidizi kwa wanawake waliokataliwa watoto wao na waume
zao na kukosa haki ya malezi ya watoto hivyo kitatoa msaada jinsi ya
kupigania haki zao.
Katika hatua nyingine kabla
ya uzinduzi huo Edna aliwashukuru wanasiasa kwa mchango wao uliomjenga
akiwezi Zitto Kabwe, Humprey Polepole na wengine waliomjenga kisiasa.
Kwa
upande wa Meneja wa Hotel ya Centre Point ambao ndio wadhamini wa
kwanza wa kipindi hicho Edwin Sigge amesema wameamua kumuunga mkono Edna
kwani anaonyesha kujituma na kuwa dhamira ya dhati kuisaidia.
Naye
Mtoto wake Edna, Lisa Brown amesema yupo pamoja na mama yake kuisaidia
jamii yenye matatizo na kwamba anamuunga mkono Rais Samia Suluhu.
No comments:
Post a Comment