Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Benki
ya Stanbic imezindua Kampeni ya Madawati Iniative huku ikibainisha
kupitia kampen hiyo itatoa madawayti 2000 kuboresha miundo mbinu ya
Sekta ya elimu nchini.
Akizungumza na
wanahabari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mkuu
wa Idara ya Wateja wa Rejareja wa benki Omari Mtiga amesema wameamua
kutoa madawati hayo kwa kuwa takwimu zinaonyesha bado kuna upungufu
mkubwa na kwamba watatoa kila mwaka kuiunga mkono Serikali.
Amebainisha
kuwa benki hiyo ina miaka zaidi ya 20 na tangu ianzishwe imeshachangia
zaidi ya Sh Bilioni moja kuchangia sekta ya afya na elimu huku akiwaomba
wadau wengine kuchangia kuboresha sekta hiyo.
"
Leo tunazindua kampeni hii mahsusi ya kuunga juhudi za Serikali
kuboresha miundo mbinu ya elimu kwa kuanzia tutatoa madawati 2000
hatutaisha hapa kila mwaka tutachangia," amesema Mtiga.
Amesisitiza
kuwa benki hiyo ina utaratibu wa asilimia moja kila mwaka kuchangia
jamii hivyo katika miaka mitano iliyopita iltoa Sh bilioni moja
kuboresha sekta ya elimu na afya.
Kwa upande
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Ndalichako ameishukuru
benki hiyo kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali kuboresha miundo mbinu
ya elimu hivyo inaonyesha jinsi gani wanavyoijali jamii.
Profesa
Ndalichako amesema bado Serikali inaendelea kuboresha miundo ya sekta
hiyo kwa kuongeza matundu ya vyoo, ujenzi wa majengo na mabweni ya
watoto wa kike na kusisitiza utaratibu wa elimu bure uanachangia
changamoto kutokana na kuongezeka kwa wanafunzi.
Naye
Mkuu wa Idara wa Masoko wa benki hiyo Desidera Mwegelo amesema wameamua
kuiunga mkono Serikali kwa namna moja au nyingine kutokana na uhitaji
wa madawati katika shule nchini na kwamba kampeni hiyo imebeba kauli
mbiu isemayo Pamoja Elimu Bora Inawezekana.
No comments:
Post a Comment