HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 15, 2021

MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MRADI NJIA KUU YA UMEME KIGOMA




Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango  akiweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa kituo cha kupoza umeme wa mradi wa njia kuu ya umeme wa kilovoti 132  unaotoka Tabora kwenda Kigoma katika eneo la Nguruka Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma.



Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango  akisalimiana na viongozi mbalimbali mara alipowasili katika eneo la Nguruka, Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma kuweka jiwe la msingi mradi wa Njia Kuu ya Umeme kutoka Tabora kwenda Kigoma.

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango   akipokea maelezo ya mradi kutoka kwa Meneja wa mradi wa Njia wa njia kuu ya kusambaza umeme wa kilovoti 132 kutoka Tabora – Kigoma Mhandisi Neema Mushi wakati wa uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huo.
Wananchi wakimsikiliza Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango katika eneo la Nguruka  Wilaya ya Uvinza  mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mradi  wa njia kuu ya kusambaza umeme wa kilovoti 132 kutoka Tabora kwenda  Kigoma Julai 15, 2021.


 

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango  akizungumza na wananchi  wa Kigoma eneo la Nguruka Wilaya ya Uvinza  mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mradi  wa njia kuu ya kusambaza umeme wa kilovoti 132 kutoka Tabora kwenda  Kigoma Julai 15, 2021. PICHA – OFISI YA MAKAMU WA RAIS

No comments:

Post a Comment

Pages