HABARI MSETO (HEADER)


July 10, 2021

MBOLEA HAI YA KIMIMINIKA YA VITALON 2000 KUONGEZA WINGI WA MAZAO SHAMBANI


Afisa mauzo wa Vitalon Agro Limited,  Bi. Cecilia Tluway akimkabidhi mbolea hai ya Vitalon Home, mmoja wa wateja waliofika kununua bidhaa hiyo.

Picha ya pamoja timu ya Vitalon Agro Limited:  (kuanzia kushoto) Mwanamina Msangi, Jilala Nkuba (Katibu wa Kampuni), Robert Mkuchu (mkuu wa kikundi cha mauzo) na Cecilia Tluway.
Afisa mauzo wa Vitalon Agro Limited, Bi. Mwanamina Msangi akionesha mbolea hai ya kimiminima ya Vitalon home namna inavyoeza kutumika kumwagilia maua ya nyumbani.

 

Na Andrew Chale, Saba Saba

MBOLEA hai ya Kimiminika kwa asilimia 100 ya Vitalon 2000 imekuwa gumzo katika maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es Salaam kutokana na ubora wake.

Banda hilo la Vitalon Agro Limited, ambalo lipo katika ukumbi (tenti) la Ali Hassan Mwinyi lifahamikalo kama banda la Kilimo ama Mtaa wa Kilimo ndio wasambazaji wakuu pekee wa mbolea hiyo hai ya Vitalon 2000 hapa nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Katibu wa Kampuni ya Vitalon Agro Limited yenye makao makuu yake Tegeta Masaiti, Bw. Jilala Kidendei Nkuba amesema muitikio wa Wananchi ni mkubwa katika kupata elimu na kununua mbolea hiyo.

"Tuna mbolea hai ya Vitalon 2000 ambapo kwa chupa moja ya ujazo wa 250 Ml inatosha kwa heka moja ambapo bei yetu ni 35,000.
Wakulima wakubwa na wadogo tunawakaribisha kuchangamkia fursa ya mbolea hii ambayo inatengenezwa Nchi za Ulaya, Jamhuri ya Czech. " Alisem Jilala Nkuba.

Jilala Nkuba ameongeza kuwa, mbolea hai ya Vitalon 2000 ni mchanganyiko wa chumvi za kikaboni, asidi ya tartaric  na citric.

"Mchanganyiko huu hulinda mmea na ina athiri  vyema usanisinuru kwenye mmea hivyo kuongeza  ukuaji  na mavuno ya mmea kati ya asilimia 24 hadi 60 pamoja na majani ya mmea." Alisema Jilala Nkuba.

Aidha, Jilala Nkuba amesema kuwa, chupa moja ya Tsh. 35,000 ambapo mtumiaji ataweka kwenye maji kati ya lita 50-100 kisha kuchanganywa kwenye dumu la ujazo la kunyunyizia  kisha tayari kwa kunyunyizia kwenye majani ya mmea ama mazao mara moja kila wiki Nne (mara moja kwa mwezi).

Mbolea hiyo hai ya Vitalon 2000 inafaida kedekede ambapo mbali na faida ya mavuno, kuna thamani na usalama mkubwa katika kutumia Vitalon 2000 ambayo ni asilimia 100 ya hai (kikaboni).

"Ni salama kutumia kati ya mifugo, wadudu wa kuchavusha na pia unapunguza kiwango cha kupakia udongo na kemikali isiyokaboni (hai). Alisema Jilala Nkuba.

Mbali na mbolea hai ya Vitalon 2000 pia wanasambaza bidhaa mbolea ambayo ipo tayari kwa ajiri ya kunyunyiza.

"Pia tuna bidhaa ya mbolea hai ya Vitalon 2000 ilikwisha andaliwa kwa ajiri ya kunyunyuzia ambayo inayofahamika kama Vitalon home (nyumbani).

Hii Vitalon home ni kwa ajili ya matumizi ya kunyunyuzia bustani za nyumbani na mimea ya ndani ya nyumba ikiwemo maua ambapo mtumiaji anaweza kutumia kunyunyizia kila wiki kwenye majani pekee.

Aidha, Jilala Nkuba amebainisha kuwa wametoa fursa kwa Vijana na  wadau mbalimbali kuchangamkia kuwa Mawakala wa mbolea hiyo ambapo amewataka kufika kwenye ofisi zao Tegeta Masaiti ama kupitia mitandao ya kijamii.

No comments:

Post a Comment

Pages