Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika banda la SUZA.
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Chuo
Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimewakaribisha na kuwashauri
wazazi walezi kutembelea banda lao la Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu,
Sayansi na Teknolojia Vyuo Vikuu wapatiwe maelekezo sahihi ya kozi
zitolewazo na chuo hicho ili waweze kuwashauri watoto wao taaluma bora
za kusoma katika mwaka wa masomo wa 2021/22..
Aidha,
chuo hicho kimewakaribisha wanafunzi waliomaliza kidato cha sita
kuhudhuria katika banda llao ili wapatiwe maelekezo ya kufanya udahili
kutoka kwa wataalamu na taaluma bora za kusoma zinazofundishwa na SUZA.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
kwenye uzinduzi wa maonesho hayo yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu
Nchini (TCU) na Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko wa SUZA, Khadija
Sadiq Mahumba.
Amesesma wazazi wataofika
katika banda lao watapatiwa elimu bora ya namna ya kuchagua kozi
zinazowafaa watoto huku akibainisha wanafunzi watapatiwa elimu bora ya
namna ya kuchagua kozi zinazowafaa kwani chuo hicho kina mazingira bora
ya kujisomea.
" Wanafunzi wahudhurie kwenye
banda letu wasiwe na wasiwasi watapata elimu sahihi ya kufanya udahili
mwaka wa masomo wa 2021/22 hata wazazi tunawashauri watembelee hapa
kuna wataalamu watawaelekeza kozi tulizonazo kwa manufaa ya watoto wao,"
amesema Khadija.
Amebainisha kuwa wanafunzi
watakaojiunga na chuo hicho watapata fursa ya kusomea taaluma mbalmbali
katika ngazi za Cheti, Astashahada, Shahada, Shahada ya Uzamili, Shahada
ya Pili ya Uzamili.
Amesisitiza kuwa chuo
hicho kinafundisha taaluma mbalimbali kwa nadharia na vitendo na kwamba
wanafunzi wataokajiunga na taaluma za afya, udaktari pamoja na upasuaji
wa meno watasoma kwa vitendo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja iliyopo
visiwani humo.
Alizitaja taaluma
zinazofundishwa na SUZA ni Kilimo, Ualimu,Utalii, Upasuaji wa meno,
ufundishaji wa Lugha ya Kiswahili na za kigeni, usimamizi wa biashara,
afya na udaktari, kompyuta, mawasiliano na uhandishi wa habari pamoja na
ufamasia.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha
Udahili wa SUZA, Ali Shauri Jecha amesema katika udahili wa mwaka wa
masomo wa 2021/22 chuo hicho kimejipanga kutoa sapoti ili kuhakikisha
wanafunzi wanafanya udahili wa vyuo na kozi kwa usahihi.
Ali
amesema watafanya matembezi katika shule lengo likiwa kuwafikia
wanafunzi wajue kozi zitolewazo na SUZA pamoja namna bora ya kufanya
udahili kupitia mtandaoni na kwamba Zanzibar wametenga dawati maalum la
kutoa elimu na udahili kwa wanafunzi.
No comments:
Post a Comment