HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 11, 2021

TANZANIA INAWAGONJWA 408 WA CORONA

 Na Jasmine Shamwepu, Dodoma


JUMLA ya wagonjwa 408 wamebainika kuwa na ugonjwa wa virusi vya Corona nchini huku wagonjwa 284  wakiwa kwenye mashine ya kupumulia ya Oxgen.

Aidha kwa takwimu za mkoa wa Dodoma zinaonyesha kuwa jumla wagonjwa 26 wana virusi vya ugonjwa wa corona  huku wagonjwa  22 wakiwa kwenye mitungi ya kupumulia ya Oxgen .

Akizungumza na wafanyabiashara katika mnada wa msalato jijini hapa Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsi Wazee na watoto Dkt Dorothy  Gwajima  amesema ugonjwa wa Corona  upo na hivyo wananchi wasichukulia mzaha katika kujikinga.

" Tuko hapa leo kwa sababu hatuhitaji kufunga biashara zenu hivyo basi tunawaomba na kuwahimiza wafanyabishara wote wa soko hili la msalato chukueni tahadhari ili tuufikie hatua ya kufunga biashara na kurudisha uchumi wetu nyuma, "   amesema  Gwajima.

Naye Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony  Mtaka amewataka wafanyabishara hao kuanzia tarehe 17 mwezi wa 7, 2021  kuhakikisha wanavaa barakoa  huku wateja wanaokuja kuhudumiwa wavae barakoa na watumie vitakasa mikono.

"Minada mingine inayofuata watu wote watakao kiuka masharti  ya kujikinga na ugonjwa wa virusi vya corona hataruhusiwa kufanya biashara au kutoa huduma katika mnada huu, Maafisa afya watatembea kibanda kwa kibanda kukagua watu kama wamevaa barakoa na kutumia vitakasa mikono na kwa yoyote atakayebainika  kuwa hana vya kujikinga kwa kweli utafungasha bidhaa zako na kurudi nyumbani ," amesema Mtaka.

Wakati huo huo Waziri na timu yake wameweza kutembea umbali wa kilomita 4 lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kuwa na mwamko wa kupenda kufanya mazoezi kwa ajili ya kuepuka virusi  vya Corona.

No comments:

Post a Comment

Pages