HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 13, 2021

TCU YAFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI KWA WAOMBAJI WA SHAHADA YA KWANZA


Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza kufunguliwa kwa dirisha la maombi ya udahili kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza.  


 

 Na Mwandishi Wetu

 

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inatarajiwa kudahili zaidi ya wanafunzi 90,000 ambapo dirisha la maombi ya udahili kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza unatarajiwa kuanza Julai 12, 2021.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa, amesema kuwa “kuanzia leo tume imefungua dirisha la maombi ya udahili kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza kuanzia Julai 12, badala ya Julai 15, 2021 iliyokuwa imepangwa hapo awali.

 

"Kufunguliwa mapema kwa dirisha hilo kunatokana na kutangazwa kwa matokeo ya mitihani ya kidato cha sita hivyo basi dirisha hilo litakuwa wazi kuanzia Julai 12 hadi hadi Agosti 5, 2021”.  alisema Prof. Kihampa.

Tume inawahimiza waombaji wote wa udahili kuendelea kupata taarifa sahihi kupitia tovuti ya TCU www. tcu.go.tz tovuti za vyuo vilivyoruhusiwa kudahili wanafunzi wa Shahada ya Kwanza, pamoja na taarifa mbalimbali zinazotolewa na TCU kupitia vyombo via habari.

Aidha tume hiyo imetoa wito kwa waombaji wa udahili na wananchi kwa ujumla kuhudhulia Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi Teknolojia yatakayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam, ambapo watapata fusa ya kuonana ana kwa ana na Vyuo via Elimu ya Juu. Maonesho  hayo yatafanyika kuanzia Julai 26-31.
 

Maombi ya Udahiii wa kujiunga na Shahada ya Kwanza utahusu makundi matatu ya waombaji ambayo ni wenye sifa stahiki za Kidato cha Sita, wenye sifa stahiki za Stashahada (Ordinary Diploma), au sifa linganifu pamoja na wenye sifa stahiki za Cheti cha Awali (Foundation Certificate) ya Chuo Kikuu Kikuu Huria cha Tanzania ambapo waombaji wanaelekezwa kusoma vigezo vilivyooneshwa katika vitabu vya mwongozo vya TCU (Undergraduate Admission Guidebooks for 2021/2022) vinavyopatikana katika tovuti ya TCU.

Prof. Kihampa aliongeza kuwa utaratibu wa Kutuma Maombi ya Udahili yatumwe moja kwa moja kwenye vyuo ambavyo muombaji amevichagua na kuchagua programu za masomo anazozipenda. Mwongozo wa programu zilizoidhinishwa kudahili na vigezo stahiki (Undergraduate Admission Guidebooks for 2021/2022) unapatikana kwenye tovuti TCU www.tcu.go.tz
 

"Masuala muhimu ya kuzingatiwa na waombaji ni kusoma mwongozo wa udahili uliotolewa na TCU kwa makini na kuelewa kabla ya kuanza kutuma maombi yoyote ya udahili, pia kuingia katika tovuti za vyuo ili mutua taratibu za kutuma maombi",  alisema Prof. Kihampa.

No comments:

Post a Comment

Pages