HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 13, 2021

MAKAMU WA PILI WA RAIS SMZ KUFUNGA MAONESHO YA SABASABA LEO

 Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam


NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo.  (Picha na Francis Dande).

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Balozi Edwin Rutageruka, akizungumza katika mkutano huo.

 

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema kuwa katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), yanayoendelea kufanyika kwenye viwanda vya Mwalimu Nyerere amesema mgeni rasmi wa kufunga anatarajiwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais  wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Abdullah.

Amesema kuwa katika Maonyesho hayo ambayo yalianza Juni 28,  hadi Julai 13 mwaka  mgeni rasmi atatoa tuzo kwa washindi was zoezi la ukaguzi wa banda bora.

Ameongeza kuwa sambamba na maonyesho hayo Utekelezaji wa miongozo na tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa w UVIKO 19 zinazotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto zinatekelezwa ipasavyo kwa kushirikiana na kamati maalumu ya kitaifa ya masuala ya afya kipindi chote cha maonyesho.

" Kupitia miongozo hii tumeweza kupunguza msongamano katika milango ya kuingilia kwa kuhamasisha watembeleaji wa Maonyesho hayo kukata tiketi kwa njia ya mtandao," amesema.

Pia ameongeza kuwa wamehamasisha watembeleaji hao kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni,kuweka vitakasa mikono maeneo mbalimbali ya uwanja pamoja na uvaaji wa barakoa.

No comments:

Post a Comment

Pages