HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 09, 2021

Wafanyabisha sasa kutumia mfumo wa taarifa za biashara



WAZIRI wa Biahara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shabaan (katikati), akizindua mfumo wa taarifa wa biashara.

 

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

WAZIRI wa Biahara na Maendeleo ya Viwanda, Zanzibar Omar Said Shabaan amesema mfumo wa taarifa wa Biashara kwa wafanyabiashara ni muhimu na kwamaba unale tija na kuondoa urasimu.

Pia utawaondolea wafanyabiashara changamoto zilizokuwa  zikiwakabili katika ufanyaji wao wa biashara na kwenda katika mabadiliko ya Teknolojia.

Akizungumza katika uzinduzi wa mfumo wa taarifa za biashara uliozinduliwa viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya 45 yanayoendelea jijini Dar es Salaam Waziri Shabaan amesema mfumo huo utaleta tija kibishara na wafanyabiashara watafurahia.

"Ni wakati wa wafanyabiashara sasa kuendana na mabadiliko ya Teknolojia hii itawasaidia kwa kiasi kikubwa," amesema waziri Shabaan.

Naye Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, amewataka wafanyabiashara kwenda na wakati na wafanye kazi kisasa kwa kutumia njia ya mtandao.

Amesema biashara kwa njia ya mtandao inasaidia kurahisisha muda na hata kupata wateja wengi tofauti na njia iliyozoeleka.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) Balozi Mteule Edwin Rutagaruka amesema mfumo huo umeshirikisha bodi mbalimbali ikiwemo bodi ya mkonge,kahawa,na korosho ili ziweze kusaidia katika ukusanyaji wa taarifa.

Ameongeza kuwa mfumo huo unaleta tija na ndio maana hivi sasa umeletwa TanTrade kwa kuwa wao ndio wadau wakubwa wa wafanyabiashara.

No comments:

Post a Comment

Pages