Baadhi ya wananchi wakipewa maelekezo katika banda la Jatu na mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Jenga Afya Tokomeza Umasikini PLC (Jatu), katika Maonyesho ya Saba Saba.
Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
WADAU na wakulima ambao wamejikita kwenye sekta ya kilimo wamesisitizwa kubeba mnyororo wa thamani kama inavyofanya kampuni ya Jenga Afya Tokomeza Umasikini PLC (Jatu), kuwawekea wakulima viwanda kila Mkoa na Wilaya wanapofanya shughuli zao.
Jatu ni kampuni ambayo inawaunganisha wakulima wadogo wadogo kufanya kilimo cha kisasa cha biashara, umwagiliaji cha mashamba makubwa.
Akizungumza leo ndani ya banda la Jatu kwenye Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maalufu Sabasaba yenye kauli mbiu ' Uchumu kwa Ajira na Biashara Endelevu' Meneja Mkuu wa Jatu Mohamed Simbano amesema wasiishie kulima wamuwekee mkulima viwanda ili aweze kuchakata na kuongeza thamani ya kile anachokilima kama serikali inavyosema.
Amesema kuwa serikali inasema kilimo kwa ajili ya maendeleo ya viwanda na kwamba serikali hii inasema kujenga uchumi wa viwanda.
Simbano ameongeza kuwa uchumi wa viwanda utakua kama kutakuwa na malighafi za viwanda na kwamba asilimia 65 ya kilimo inachangia ajira na asilimia 30 pato la Taifa.
Ameeleza kuwa kilimo ni moja ya sekta ambayo inanyanyua uchumi wa Taifa wadau hao wa kilimo wanatakiwa kubadilisha mawazo ya kulima na badala yake wafikirie namna ya kuleta mnyororo mzima wa thamani katika kilimo.
Simbano amesema Jatu inafanya miradi ya kilimo katika mikoa ya Manyara wilayani Kiteto ambapo ina lima mahindi na alizeti, Morogoro Wilaya ya Kilosa wanalima zao la mpunga, Tanga maharage na machungwa, Njombe parachichi, Tarime Mkoa wa Mara ndizi na ngano na Dar es Salaam Wilaya ya Kigamboni mbogamboga.
" Kila Mkoa tunapolima mazao yetu tuna viwanda vya kuchakata malighafi kwa ajili ya kutengeneza mnyororo wa thamani na mkulima aweze kupata faida lakini pia kuwanufaisha vijana wazawa kwa kupata ajira pindi wanapoendesha viwanda hivi " ameongeza.
Huwezi kumiliki miradi ya Jatu kama si mmiliki wa kampuni hiyo mlango pekee wa kumiliki ni kununua hisa ambayo zinaanzia kumi kwa shilingi 5000 na thamani ya hisa moja ni shilingi 500," amesema Simbano.
Amesema zoezi la uuzaji wa hisa za Jatu linafungwa rasmi Julai 15 mwaka huu hadi watakapopewa kibali cha kuuza tena na serikali.
No comments:
Post a Comment