Waziri
wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho amezindua Bodi ya
Wakurugenzi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) na kuiagiza
bodi hiyo kutatua haraka changamoto za kiutendaji zinazohusiana na
majukumu ya kibiashara ili kuwapatia wateja huduma bora na zenye
gharama nafuu.
Akizindua bodi hiyo leo jijini
Dar es Salaam Waziri Dkt Chamuriho amesema bodi iliyomaliza muda wake
ilitekeleza majukumu yake ipasavyo na kwamba changamoto hiyo ipo hivyo
bodi iliyoteuliwa inatakiwa kuitatua lengo likiwa kuwapatia wadau wake
huduma bora.
" Naomba nitumie fursa hii
kuiagiza bodi ya TASAC changamoto hii iwezekanavyo tunaamini iliyopita
ilitekeleza majukumu lakini bado kuna malalamiko mkiitaua wateja
watapata huduma bora na gharama rafiki, " amesema Waziri Dkt. Chamuriho.
Waziri
huyo ameiagiza bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo kutatua chanagamoto
za kisheria kwa kushirikiana na wadau kisha kuwasilisha maoni wizarani
na kwamba zinazohusu Bunge zifikishwe kwa mujibu na tatratibu zilizopo.
Ameisisitiza
bodi hiyo kuhakikisha inasimamia matumizi ya rasilimali za umma kama
ilivyoelekezwa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiwaapisha Makatibu
Wakuu wa wizara hiyo Aprili 6 mwaka huu.
Ameikumbusha
bodi hiyo kusimamia majukumu yake ipasavyo kama ilivyoanishwa kwenye
sheria iliyoanzishwa na TASAC ambayo ni kuisimamia menejimenti ya
shirika hilo.
Katika hatua nyingine Waziri Dkt.
Chamuriho ameisisitiza bodi na menejimenti ya TASAC kuzingatia
miongozo inayotolewa na Msajili wa Hazina, kujaza muundo wa utumishi na
kuutekeleza, kutekeleza mikataba ya utendaji wa msajili, mkurungenzi
mkuu wa TASAC na Katibu Mkuu, kuandaa programu ya shughuli za bodi xza
kila robo mwaka na kuzisimamia pamoja na kufuata sheria na kanunia bila
upendeleo kwa watoa hduma na wateja.
Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo (Uchukuzi) Gabriel Migire amesema mchakato wa uteuzi
wa wajumbe wa bodi ya TASAC uliofanyika kwa umakini na kuitaka
kutekeleza majukumu yake kulingana na mipaka yeake sio kuingilia ya
menejimenti.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi
hiyo Kapteni Mussa Mandia amesema watatekeleza maagizo yote
yaliyotolewa kwa wakati ili kuhakikisha malengo yanafikiwa
Naye
Mkurugenzi wa TASAC Kaimu Mkeyenge amewapongeza wajumbe wa bodi
walioteuliwa na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano kuhakikisha malengo
yaliyowekwa na shirika yanafikiwa kwa masilahi ya taifa.
Wajumbe
saba walioteuliwa ni Rukia Shamte, Said Nzori, Said Kiondo, Mhandisi
Aron Kisala, Kapteni King Chiragi ,Cassian Ngamilo pamoja na
Mwenyekiti Kapteni Mandia.
No comments:
Post a Comment