HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 01, 2021

Waziri Gwajima atuma salamu kwa walioiba mabilioni ya pesa za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya

 


 

Na Jasmine Shamwepu, Dodoma

 

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema kuwa ubadhirifu na wizi uliofanywa katika kipindi cha miaka mitatu kutokana na watu kughushi mabilioni ya pesa kwenye mfuko wa bima ya afya ili walipwe malipo yasiyo halali salamu ziwafikie popote walipo  walale wakiwaza kulipa fedha walizoiba.


Kauli hiyo aliitoa leo  jijini Dodoma wakati akizindua bodi mpya ya wakurugenzi wa mfuko wa Bima ya Afya na maadimisho ya miaka 20 ya mfuko huo ambapo alisema kuwa watu hao wawekewe mpango wakuzilipa kiambatisho na mpango wa uwajibikaji.


"Imefika wakati kukiwa na mabadiliko kwa manufaa ya nchi haijalishi kama watu watakuchukia wanaoanza kazi waanzie hapo kwani nyakati na maono yana mabadiliko ili kufikia malengo kwa kasi huru"amesema Dkt. Gwajima.



Alisema kuwa bodi imekuja wakati wizara ya Afya inakusudia kuwasilisha muswada wa sheria ya Bima ya Afya Bungeni kuhusu kusimamia utekelezaji wa Sheria hiyo muhimu.



Alisema utekelezaji wa jambo hilo unaendelea vizuri,tayari kwenye bajeti ya Serikali mwezi Juni zoezi hilo linatekelezwa ambapo bil149 zitatolewa kwa wasio na uwezo wa kulipia bima ambapo Septemba Mwaka huu Muswada unaenda Bungeni.



Alisema kuwa anatambua jitihada zilizofanyika za watu kujiunga na bima hadi kufikia wanufaika milioni4.


"Asilimia 80 ya watanzania waliojiunga ni ndogo hivyo waweke mikakati njia za kuwafikia kwa haraka wananchi kwenye huduma ya Bima ya Afya hasa Vijijini hebu watumie taaluma na Teknolojia nzuri kwa kushirikiana na Wizara ya mawasiliano kufikisha Habari ya huduma ya Bima ya Afya kutokana na Watu kutokujua bima kwani watanzania wengi wanaishia kutoa hela nyingi hospitali kutokana na kukosa Bima”alisema.


Pamoja na hayo alisema kuna maagizo mahususi yanayotolewa na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii wakamilishe fao la Wazee wastaafu kuingia kwenye bima.


"Kuongeza wategemezi ni suala muhimu kwani limewaondolea mzigo wazazi na walezi"amesema .


Wakati huohuo Dkt.Gwajima amesema watu wa kwenye vituo vya Afya  uwajibikaji wao ni mbovu kwani hawapendi kukopa pesa kwaajili ya kununua dawa na vifaaa na hivyo kushindwa kuwahudumia wateja waliojiunga na bima hivyo suala hilo ni tatizo.


"Wanaona wakiboresha kituo cha Afya kwa Bima duka la dawa la mfukoni litakufa Watu hawa hawafai kwenye uongozi hivyo nakuelekeza Katibu Mkuu kawaondoe watumishi hao kwani hawawezi kuvumilia mambo hayo"alisema.


Pamoja na hayo alimuagiza Mwenyekiti wa Bodi mpya kuwa suala la uzembe wa kudhoofisha mifumo ya Bima ya Afya wamefanya utafiti kukosea kujaza fomu za bima,kwani utafiti unaonyesha kiasi cha bil.6.1 zimekatwa katika hospitali za Mikoa kwa miezi18 nakusema kuwa mifumo iliyopo itawasaidia kuondoa hilo.



Wakati huo huo Dkt. Gwajima aliwataka MSD na Bima waweke mfumo wakufanya kazi pamoja,hivyo waainishe vikwazo vilivyopo ili viweze kuondolewa.



Pamoja na hayo aliitaka bodi hiyo kuifanyia kazi ripoti ya mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) na kila mwanataaluma aliyosaini atendewe haki nilIShasema siwezi kuvumilia baadhi ya Watu waongo na wezi Rais ameshasema Serikali ya awamu ya sita hatutaki mchezo,tutakwenda hivyohivyo na mwishoni tutawanyang'anya leseni.
 


Lazima tujue kutunza Fedha vizuri Kama tunataka bima iendelee,Katibu Mkuu na Mkurugenzi wawasilishe mpango ,nakusema kuwa Sera iliyopo isife kwani hata Sheria ikija wizi ni uleule.


Mifumo ya TEHAMA Kuna baadhi ya Watu hawaitakii mifumo hiyo hivyo anaetakiwa kufunga mifumo ya TEHAMA  wafanye hivyo lazima wawambie mpango upi utawafanya kufika Septemba Bodi pia waangalie hilo ili mifumo ifungwe.


Waendelee kubuni mbinu bora za kufanya tathmini ili kuondoa malalamiko pia watanue wigo wa huduma ambao hautaua mfuko bali utaendeleza mfuko ifikapo Augost watangaze kutita kipya.


Alisema maadhimisho ya miaka 20 ya NHIF,Serikali ya awamu ya sita imejipambanua kwa falsafa ya kazi iendelee hivyo nao wajielekeze kuweka mifumo bora ya kuendeleza kazi na kuhakikisha wanawafikia wanancha kwa kusikiliza kero zao.


"Wekeni mpango madhubuti wakushughulikia changamoto mbalimbali lakini bado Watu hawaijui bima,hivyo katoeni elimu zaidi kwa wananchi kwakutumia viongozi wa mitaa,kata na vijiji ili kuona umuhimu wa Bima na kujiunga.

 

Kwa  upande  wake naibu waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt.Godwin Mollel alisema kuwa watakaa chini kuweka mambo sawa ambapo watahakikisha watanzania wanapata huduma halisi kitu ambacho anataka Rais,na watanzania wanataka haki na Uhuru wa Watu .


Alisema kazi nyingine watakayoifanya ni kutaka kujua mfumo mzima wa Bima hadi chini kujua watumishi gani wanatumia muda kwenda kutibu.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Prof. Abel Makubi alisema kuwa Bodi mpya itaendeleza mazuri yote yaliyofanywa na Bodi iliyopita ingawa bado kuna mambo mengi yakufanyiwa kazi hasa kuhusiana na wanachama ambapo bado wananchi wanatamani kuona mfuko wa bima ya afya unaboresha huduma zake huku akizitaka Bodi mpya kubuni Mambo mapya na kuona wananchi wanafurahia huduma hiyo.


"Watumishi nao wana changamoto zao hivyo Bodi nendeni mkawasaidie kuzitatua changamoto hizo"alisema.
 

Awali  mwenyekiti wa Bodi NHIF Anna Makinda ,alisema kuwa amefurahi kuwa sehemu ya miaka 20,kwani wameweza kukarabati muundo wa NHIF,kutengeneza saikolojia,walipunguza kurugenzi ya NHIF ili kuanza upya,na kuitaka bodi hiyo mpya kwenda kusimamia suala la TEHAMA ili kuondoa masuala ya rushwa.


"Tuliona bima ni muhimu kwa kila mtu na ndio maaana kulianzishwa vifurushi kwa wananchi wote"alisema Makinda.



Pia alisema walisimamia suala la uadilifu wakagundua kuwepo kwa suala la udanganyifu miongoni mwa watumishi wa NHIF.


Mkurugenzi mkuu wa NHIF Benard Konga amesema uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF,kama mfuko wamekuwa wakiboresha utoaji huduma za kibingwa ikiwemo  moyo,Figo


Alisema changamoto iliyowaweka katika hali ngumu ni ucheleweshwaji wa kulipa madai,tayari vituo 40 vimejisajili.



"Natoa rai kwa watoa huduma watumie mfumo huo ili kumaliza malalamiko yanayotokana na madai"alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages