Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Dkt. John Mduma (kulia), akimsikiliza mwananchi aliyetembelea banda la Mfuko viwanja vya Sabasaba.
Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
MKURUNGEZI wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma amesema kuwa marekebisho makubwa waliyayafanya mwaka huu ni kupunguza kiwango ambacho waajiri wa sekta binafisi walikuwa wakichangia asilimia moja ya mshahara na kufikia asilimia 0.6.
Akizunguma jana katika banda la mfuko huo kwenye maonyesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam(DITF), Muuguzi katika chumba cha amsema kuwa sekta ya Umma imekuwa ikiendelea kuchangia asilimia 0.5 ya mshahara.
Mkurugenzi huyo amesema kuwaa sekta ya Umma haijabadilishiwa kiwango cha uchangiaji katika marekebisho yaliyofanyika
Amesema kuwa madhumuni ya kupunguza sekta binafisi mchango huo ni ili kuhakikisha wanaipa uhuru sekta hiyo kuendelea kukua kwa kasi katika uchangiaj ajira na uchumi.
" Na hii ni dhana kamali ya utekelezaji wa kitabu cha marekebisho kuhakikisha sekta hinafisi inakua kwa kazi " amesema.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Takwimu katika mfuko huo James Tenga amesema wapo katika maonyesho hayo kuwaelimisha wateja wao na waajiri namna gani mfuko wa WCF unavyofanya kazi na kuishi kaulimbiu ya mwaka huu inayosena ' Uchumi wa Viwanda Ajira kwa vijana na Biashara Endelevu'.
Tenga ameeleza kuwa Serikali imeamua kupunguza kiwango cha uchangiaji kwa waajiri wa sekta binafisi na kwamba hiyo itasaidia katika kuboresha biashara hapa nchini.
" Hi itasaidia kuleta fursa kwa waajiri kuweza kuongeza ajira kwa wafanyakazi na kuwaboreehea maslahi yao. Tunawaeoimisha wateja wetu pamoja na napunguzo haya nfuko huu bado utaendelea kuwa endelevu" anesema Tenga.
Ameongeza kuwa mfuko unawekeza katika uwekezaji unaoendana na kaulimbiu ya maonyesho hayo na kwenye viwanda unatoa ajira kwa maeneo mbalimbali kwa wafanyakazi walioajiri.
Ameongeza kuwa wanatoa ajira kwa wakulima ambao wanazalisha mazao mbalimbali ambao mfuko huo unatumia katika viwanda hivyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Tathimini katika mfuko wa fidia kwa wafanyakazi Dkt. Msalamu Omary amesema kutengo chake ni katika masuala kufanya Tathimini kwa walemavu.
" Tathimini tulizofanya ili mfanyakazi aweze kupata mafao mbalimbali ya fidia na Kuna takribani ya mafao hayo Saba " amesema Omary.
Amebainisha kuwa moja ya mafao hayo ni mfanyakazi atakapopata ulemavu wa kudumu akawa hawazi kujisaudia mfuko utanuwekea mtu wa kumuhudumia kwa maisha yake yote.
No comments:
Post a Comment