....Ni za umahiri za Euromoney na Global Banking
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo ya
umahiri ya Euromoney kama Benki Bora Tanzania 2021 na Benki bora huduma
kwa wateja binafsi na Biashara wakati wa hafla
iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Fedha,
Juma Kimori na Mjumbe wa Bodi
ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. George Mulamula.
Mjumbe wa Bodi
ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. George Mulamula, akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kupokea tuzo ya umahiri ya Euromoney kama Benki Bora Tanzania 2021 na Benki
bora huduma kwa wateja binafsi na Biashara. Kushoto ni Afisa Mkuu wa
Fedha, Juma Kimori.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna akimkabidhi Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dkt. George Mulamula, Tuzo ya umahiri ya Euromoney kama Benki Bora Tanzania 2021 na Benki bora huduma kwa wateja binafsi na Biashara wakati wa hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna pamoja na Mjumbe wa Bodi
ya wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. George Mulamula, wakifurahia kupokea
Tuzo ya umahiri ya Euromoney kama Benki Bora Tanzania 2021 na Benki
bora huduma kwa wateja binafsi na Biashara wakati wa
hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mkuu wa
Biashara na wateja binafsi, Filbert Mponzi na Kushoto ni Afisa Mkuu wa
Fedha, Juma Kimori.
NA MWANDISHI WETU
BENKI
ya NMB, imeshinda tuzo mbili za kimataifa ‘kwa mpigo,’ za Benki Bora
Tanzania na Benki Bora ya Huduma kwa Wateja Binafsi na Biashara za Kati,
Tanzania, zilizotolewa na majarida maarufu yanayoangazia huduma za
kifedha duniani.
Jarida
la Euromoney limeitangaza NMB kuwa mshindi wa Tuzo ya Benki Bora
Tanzania kwa mwaka wa tisa mfululizo, huku Global Banking and Finance,
likiitaja kama Benki Bora ya Huduma kwa Wateja Binafsi na Biashara za
Kati nchini.
Akizungumza
wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo hizo kwa Bodi ya Wakurugenzi wa NMB,
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa benki hiyo, Ruth Zaipuna, alisema NMB
inajivunia ufanisi uliozaa tuzo hizo, huku akitaja siri za mafanikio
hayo.
Akimkabidhi tuzo
hizo Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NMB, Dk. George Mulamula, Zaipuna
alisema ubunifu wa bidhaa, uwekezaji kiteknolojia na suluhu za
kidigitali ni kati ya mambo yaliyochangia kuifanya NMB kuwa benki bora.
Zaipuna
aliongeza kuwa, tuzo hizo kutoka Euromoney na Global Banking and
Finance, majarida yenye Makao Makuu London, Uingereza, ni kielelezo kuwa
juhudi za benki zinatambuliwa si tu Tanzania, bali hata na taasisi za
kimataifa..
“Ni heshima
na mafanikio makubwa kwa NMB kupata tuzo hizi. Tunajivunia kuona juhudi
zetu zinatambuliwa kimataifa na tunajiona tuna deni la kuendelea
kujituma zaidi ili kubaki kwenye viwango vya kimataifa kama benki bora,”
alisema.
Akipokea tuzo
hizo, Mulamula aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Edwin Mhede,
alisema tuzo hizo zina maana kubwa kwao, huku akiupongeza uongozi wa
benki hiyo na wafanyakazi kwa mafanikio hayo na kuwataka kutobweteka.
“Naipongeza
menejimenti na wafanyakazi kwa utendaji wao mzuri uliosababisha ushindi
huu. Tuzo ya Euromoney ni ya mwaka wa tisa mfululizo na pia Global
Banking and Finance kuitambua NMB kama Benki Bora ya Huduma kwa Wateja
Binafsi na Biashara za Kati.
“Ningependa
ieleweke kwa jamii na wateja wetu kuwa, tuzo hizi zina maana moja kubwa
kwamba NMB ni benki bora hapa Tanzania na tumejikita katika kutoa
huduma bora kwa Watanzania magali popote walipo mijijini na vijijini.
“Nawashukuru
wateja na Watanzania kwa kuifikisha NMB hapa, wajibu wetu ni kuendelea
kuwa benki bora inayoakisi kasi ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Uongozi na wafanyazi wasibweteke, waongeze ufanisi ili kubaki juu kwa
ubora,” alisema Zaipuna.
Tuzo
hizo zimetolewa kwa kuzingatia vigezo kadhaa kwa benki
zilizopendekezwa, ukiwamo ufanisi wa mahesabu na utendaji kwa ujumla,
mkakati wa huduma za kidijitali, huduma jumuishi za fedha, usalama wa
huduma za kimtandao na uwajibikaji wa benki katika jamii inayoizunguka.
Vigezo
vingine vilivyotumika ni mtaji wa benki, mapato yatokanayo na mali za
kampuni, pato litokanalo na riba, uwiano wa fedha na gharama za
uendeshaji, kiwango cha amana za wateja na kiwango cha mikopo katika
soko.
Pia limo vigezo vya
uwiano kati ya mikopo na amana za wateja, uwiano wa mikopo chechefu, na
uwiano wa hasara itokanayo na mikopo chechefu.
No comments:
Post a Comment