Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na waandishi wa habari.
Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Akizungumza
na wanahabari jijini Dar es Salaam alisema wanachama wa CHADEMA
wanapaswa kuelewa mwenyekiti wao si malaika bali ni binadamu anayeweza
kutenda kosa la uhalifu na kwamba kufanya maandamano ni kuvunja sheria
hivyo wanatakiwa kusubiri mahakama itoe uamuzi.
"
Wanachama wajue Mbowe si Malaika ni binadamu anayeweza kufanya uhalifu
kama ni mkweli anamwogopa Mungu waende kumuuliza atawaeleza ukweli,"
amesema IGP Sirro.
Amebainisha
mwaka jana kabla Uchaguzi Mkuu aliweka wazi kuna watu wanapanga njama
za kulipua visima vya mafuta pamoja na kufanya mauaji ya viongozi na
kusisitiza kuwashughulikia kabla hwajafanya matukio hayo hivyo tayari
jeshi hilo limeshawasilisha ushahidi kinachosuburiwa mahakama itoe
uamuzi.
Ameongeza
kuwa polisi hawamwonei Mbowe bali linafuata sheria kwa watu wanaotaka
kuharibu amani na utulivu kwa manufaa yao na kuzikosoa asaki za kiraia
na viongozi wa dini wanaosema mwanasiasa huyo anaonewa.
Amefafanua
kuwa jeshi hilo haliwezi kuwaacha watu wachache wafanye nchi isikalike
kwa kuendekeza tamaa zao na kwamba watakaokaidi utii wa sheria
watachukuliwa hatua.
Aidha,
amewaonya watu kutoka mikoani walioandaliwa kufanya maandamano
kutofanya hivyo kwani polisi halitawavumivilia kwa kuwashughulikia
kikamilifu.
Katika
hatua nyingine, IGP Sirro ametoa maagizo kwa makamanda wote wa mikoa
kufanya oparesheni ya mwezi mmoja ya kuwakamata na kuwachukulia hatua
madereva Bodaboda wanaokiuka sheria na kanuni za usalama barabarani
ikiwemo kutovaa kofia (Helmet), kupakia mishkaki pamoja na abiria
kutopewa kovia.
Amesema
wameshajitahidi kutoa elimu kwa madereva hao ila kuna baadhi wasiotii
sheria kusababisha ajali nyingi kutokea hivi karibuni.
Wakati
huo huo, ameziomba halmashauri kutunga sheria ndogo ndogo
zitakazowabana watu wanaokataa kuchangia fedha za ulinzi shirikishi na
kuzipongeza halmashauri ya Ubungo na Kinondoni kwa kuwa na sheria hizo.
No comments:
Post a Comment