Mwenyekiti wa Bodi ya ERB, Profesa Ninatubu Lema akizungumza na wahandisi vijana kwenye Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.
Msajili
wa Bodi ya Wahandisi (ERB) akizungumza na wahandisi vijana kwenye
Kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee wilayani Ilala
jijini Dar es Salaam.
Wahandisi Vijana wakiwa kwenye Kongamano liloandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), lilifanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.
Wahandisi
Vijana wakiwa kwenye Kongamano liloandaliwa na Bodi ya Usajili wa
Wahandisi (ERB), lilifanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee wilayani Ilala
jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
RAI imetolewa kwa vyuo vinavyofundisha masomo ya uhandisi nchini kuongeza udahili wa wanafunzi ili kukidhi hitaji la soko.
Ombi
hilo limetolewa na Msajili wa Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB),
Mhandisi Patrick Barozi wakati wa mjadala wa Kongamano la Wahandishi
Vijana lilifanyika jijini Dar es Salaam.
Mhandisi
Barozi alisema ERB hadi sasa imesajili wahandisi 31,729 wanawake wakiwa
3,344 idadi ambayo ni ndogo kulingana na hitaji lao kwa jamii.
Alisema
kulingana na idadi ya Watanzania idadi hiyo haitoshi kutekeleza miradi
hivyo ni jukumu la vyuo vinavyofundisha masomo hayo kuongeza udahili.
"Hadi
sasa ERB imesajili wahandisi 31,729 ambao wamehitimu kwenye vyuo vyetu
kama Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
Kitivo cha Uhandisi (CoET), Taasisi ya Tenkolojia Dar es Salaam (DIT),
Chuo cha Ufundi Arusha, Chuo cha St.Joseph na vingine," alisema.
Msajili
alisema iwapo vyuo hivyo vitaongeza udahili Tanzania itakuwa na
wahandisi wengi wa fani mbalimbali ambao watasaidia kwenye uzalishaji na
kukuza uchumi.
Alisema
wameamua kuandaa kongamano hilo la wahandisi wa vijana ili kuwawezesha
kubaini fursa na changamoto katika kufanikisha mapinduzi ya nne ya
viwanda.
Barozi
alisema kongamano hilo lililenga kuonesha umma kundi hilo muhimu kwa
maendeleo ya nchi na kuleta tija kwa vijana wahandisi.
"Pia tunaamini jukwaa hilo litachochea bunifu mbalimbali zinazobuniwa na vijana hao na namna ya kuziendeleza," alisema.
Barozi
alisema wahandisi vijana wamekuwa wakitumika katika miradi mbalimbali
kama ujenzi wa reli, madaraja, barabara, viwandani, umeme na maji jambo
ambalo linatoa matumaini.
Alisema
kauli mbiu ya kongamano hilo ni fursa na changamoto kwa mhandisi kijana
katika kufikia mapinduzi ya nne ya viwanda, hivyo ni imani yao ni kuona
vijana hao wananufaika nayo.
Msajili
alisema ERB imejipanga kuandaa kongamano la wahandisi vijana kila mwaka
ili kuwaandaa kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kabla ya
kuajiriwa au baada ya kuajiriwa.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya ERB, Profesa Ninatubu Lema aliwataka
wahandisi hao kujiuliza watafanyia nini jamii ili kuchangia mabadiliko
ya kiuchumi, viwanda na maendeleo.
Alisema
wahandisi vijana ni kundi muhimu katika kuchochea mabadiliko na
maendeleo nchini hivyo wakiamua kutumia taaluma zao kwa weledi mafanikio
yatapatikana.
"Napenda
kuwaasa vijana wangu mfanye kazi kwa uhakika ili uache alama
itakayokumbukwa milele na sio kukimbilia kujinufaisha wenyewe," alisema.
Mwenyekiti
huyo alimtolea Mhandisi Lulu Dunia ambaye anasimamia Mradi wa Daraja la
Tanzanite kuwa ameonesha mafanikio makubwa hivyo anapaswa kuigwa.
Wakizungumzia
kongamano hilo wahandisi vijana Samwel Sumari, Neema Njanga, Emmanuel
Lazaro na Getrude Christopher wamesema ni muhimu kwao na linapaswa kuwa
endelevu.
Wahandisi
hao wamesema kongamono hilo limewafungua kwa kutambua fursa zilizopo
kwenye sekta hiyo na namna ya kujiajiri ili kusaidia kukuza uchumi na
maendeleo nchini.
No comments:
Post a Comment