Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mikutano wa JNICC.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mussa Zungu akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Stargomena Tax akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku ya tano ya kamati hiyo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa JNICC.
Waziri wa Ulinzi wa Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stargomena Tax akiwa katika pich aya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo mara baada ya kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stargomena Tax amefunga
Mafunzo ya Siku Tano ya Diplomasia ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya
Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama huku akibainisha kuwa wajumbe wa kamati
hiyo kuyatumia kuimarisha diplomasia ya uchumi na kulinda maslahi ya
nchi.
Ameyasema hayo leo jiijini Dar es Salaam
wakati akifunga mafunzo hayo kwa wajumbe wa kamati hiyo yaliyofanyika
Katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC).
Amesema
kuwa mafunzo waliyopatiwa wajumbe ni maalum kwa kuendeleza uchumi wa
nchi na kwamba yatawaongezea maarifa katika masuala ya kulinda asilahi
ya kijamii na kiusalama hivyo yana tija kubwa kwa taifa.
"
Mafunzo hayo ni muhimu kuendeleza uchumi wa nchi kwani diplomasia
inategmea ulinzi na usalama nina imani mtayatumia kutetea masilahi
mapana ya nchi na kuchochea maendeleo ya uchumi," amaesma Dkt. Tax.
Amebainisha
kuwa kamati hiyo ina jukumu la kuhimiza matumizi ya sahaihi ya mitandao
na teknolojia kwa ajili ya kuleta maendeleo kwani isipotumika vyema
inawaeza kuhatarisha amani na usalama wa nchi.
Amemshukuru
Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini na kumteua waziri wa wizara na
kwamba atatekeleza majukumu yake kwa weledi na kuzingatia sheria n
taratibu zilizowekwa.
Kwa upande wake Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano w Afrika Mashariki Balozi
Joseph Sokoine amesema mafunzo yalilenga kuwajengea uwezo wajumbe katika
masuala ya diplomasia ya uchumi, usalama wa nyaraka za ubalozi na
kwamba wabunge wamaejadili na kutoa mapendekezo kwa wizara.
Nae,
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mussa Zungu amemuomba katibu wa wizara hiyo
kuongeza maafasa biashara kwenye balozi au kufungua vituo vya biashara
katika balozi wanazoziwakilisha
Amempongeza
Rais Samia kwa namna anavyoshughulikia masuala ya nchi ikiwemo dhamira
yake ya dhati kuifikisha nchi kati ka uchumi wa juu wa kati.
Amefafanua
kuwa nchi haiwezi kukwepa kushirikiana na mataifa ya nje katika
uwekezaji na miradi ya kimkakati kwani inasaidia nchi kupata teknolojia
mpya na ubunifu.
No comments:
Post a Comment